Pata taarifa kuu

Al Shabab yadai kushambulia kambi ya jeshi Galgaduud na kuua askari kadhaa, jeshi lakanusha

Magaidi wa Al Shabab, wameshambulia kambi ya jeshi katika jimbo la kati la Galgaduud na kusababisha makabiliano makali mapema hivi leo. 

Somalia inaendelea kuathirika kutokana na mizozo ya kisiasa isiyoisha.
Somalia inaendelea kuathirika kutokana na mizozo ya kisiasa isiyoisha. REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea alfajiri ya leo katika kambi hiyo iliyo kwenye kijiji cha Qayib, na ripoti zinasema, walikuwa wamejihami kwa mabomu ya kujitoa mhanga. 

Hili ni shambulio linalokuja, katika kipindi ambacho jeshi la Somalia limeonekana kufanikiwa kudhibiti maeneo ya jimbo hilo, lililokuwa linadhitiwa na magaidi hao. 

Waziri wa Habari katika jimbo la Galgaduud, Ahmed Shire Falagle amesema jeshi la serikali likishirikina na wapiganaji wa kijiji walifanikiwa kuwafukuza magaidi hao na hali ni utulivu katika eneo hilo. 

Hata hivyo, upande wa Al Shabab unadai kuwauawa wanajeshi wa serikali lakini upande wa serikali unasema, magaidi 15 wameuawa katika makabiliano hayo. 

Tangu mwaka 2006, kundi la Al Shabab, limesababisha maelfu ya watu nchini Somalia, katika jitihada za kupindua serikali mjini Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.