Pata taarifa kuu

Wakimbizi wa Kisomali nchini Kenya: Hali mbaya katika kambi ya Dadaab

Milioni moja ni idadi ya Wasomali waliofukuzwa kutoka makwao kutokana na ukame tangu mwanzoni mwa mwaka kulingana na Shirka la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, UNHCR. Wengi wametoroka nchi yao, wengine nchi jirani. 

Mwanamke wa Kisomali ambaye ni mkimbizi wa ndani karibu na mzoga wa mnyama aliyekufa kutokana na ukame mkali unaotokea mara kwa mara, katika eneo la Gedo nchini Somalia, Mei 26, 2022.
Mwanamke wa Kisomali ambaye ni mkimbizi wa ndani karibu na mzoga wa mnyama aliyekufa kutokana na ukame mkali unaotokea mara kwa mara, katika eneo la Gedo nchini Somalia, Mei 26, 2022. © FEISAL OMAR/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika kambi ya Dadaab ya watu waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Kenya, watu wapya 300 wa Somalia waliokimbia makazi wanawasili kila siku, sawa na watu 20,000 zaidi katika miezi miwili iliyopita. Matokeo: mashirika ya kiutu yako chini ya shinikizo na hali mbaya ya maisha.

Ilikuwa imepita muda mrefu kambi ya wakimbizi ya Dadaab haijawapokea wakimbizi wengi, anasema Jamin Kusuania, afisa wa shirika lisilo la kiserikali la IRC.

"Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita ambapo tumeona watu wakiwasili kwa wingi huko Dadaab. Kwa kiwango hiki tunatarajia kupokea watu wengi zaidi kuliko wakati wa njaa ya miaka ya 2011 hadi 2012. "

Katika kambi ya Dadaab, msongamano na ukosefu wa ufadhili ni matatizo ya kudumu, yanayochangiwa na wimbi hili jipya la wakimbizi, ambao wako hatarini zaidi, mara nyingi hawana chanjo au hawajachanjwa, mara nyingi na wakati mwingine wanakabiliwa na utapiamlo.

"Ni vigumu kusema ni wangapi kati ya wanaowasili wana utapiamlo, lakini ni ugonjwa ambao umeenea sana. Hili ni moja ya matatizo makubwa tunayokumbana nayo”.

Tangu 2015, Kenya haisajili tena wakimbizi kutoka Somalia. Bila hati za utambulisho, wananyimwa huduma fulani, huduma, au mpango wa usaidizi kwa waliohamishwa. Kwa hivyo IRC inataka kila kitu kifanywe ili kuwaruhusu kusalia nchini mwao.

"Mgogoro wa kweli unakuja kama hatuwezi kupata nafasi ya kuhudumia watu hawa au kukabiliana na tatizo nchini Somalia, ili watu wasilazimike kuvuka mpaka. "

Kulingana na vyanzo vya habari, majadiliano yanaendelea kati ya UNHCR na mamlaka ya Kenya, ili kufungua tena moja ya maeneo ya watu waliokimbia makazi yao huko Dadaab, yaliofungwa miaka kadhaa iliyopita kufuatia kurejeshwa kwa maelfu ya wakimbizi nchini Somalia. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, akiwa ziarani nchini Somalia na Kenya, Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi, alijadiliana na Rais William Ruto kuhusu mahitaji ya maendeleo ya kambi za wakimbizi nchini humo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.