Pata taarifa kuu

Mzozo Tigray: Serikali ya Ethiopia yashambulia tume ya Umoja wa Mataifa

Nchini Ethiopia, hali inaonekana si nzuri kwenye uwanja wa vita katika jimbo la Tigray, ambako vita bado vinaendelea kwa wiki ya pili. Kwa upande wa kisiasa, hata hivyo, serikali ya Ethiopia imejibu kwa maneno makali, Ijumaa hii, Septemba 9, kwa tamko jipya, Jumatano, la wataalam wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uchunguzi wa hali ya mambo nchini Ethiopia

Gari lililoharibiwa kando ya barabara katika Jimbo la Tigray.
Gari lililoharibiwa kando ya barabara katika Jimbo la Tigray. © RFI/Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia inasema "imesikitishwa" Ijumaa hii asubuhi, na haikutaka kukaa kimya. Kulingana na serikali ya Ethiopia, wataalam wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa "hawana umahiri wala kuthamini mzozo uliochochewa na waasi wa TPLF kwa kukiuka makubaliano ya kibinadamu".

Serikali ya Ethiopia imetaja wito wao wa kuchukua hatua kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama "dhahiri chuki dhidi ya Ethiopia". Imeongeza kwamba, "amani na usalama" havishughulikiwi na mamlaka yake.

Kinachoonekana kuikasirisha serikali ya Ethiopia ni kwamba wataalamu hao Jumatano, kwa mara ya pili tangu kuanza kwa mapigano Agosti 24, waliwashutumu wapiganaji kutoka pande mbili, huku Ethiopia ikijiona kuwa imeshambuliwa. Na pia wataalamu hao wamedai kwamba Eritrea"inashiriki katika uhasama" na kwamba mzozo huo unaweza "kuenea katika nchi zingine".

Vita hivi vya maneno vinatokea wakati huko New York, nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikubaliana kujadili vita nchini Ethiopia baada ya majadiliano makali. Mkutano, ulioombwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ireland, Norway na Albania, hatimaye utafanyika Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.