Pata taarifa kuu

Marekani yatuma Mjumbe wake kwa Pembe ya Afrika nchini Ethiopia

Eneo la Kaskazini mwa Ethiopia linaendelea kukumbwa na hatari kubwa. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilichukua mkondo mpya wiki hii kwa kuingia kwa Eritrea katika vita huko Tigray, dhidi ya waasi wa TPLF. 

Mike Hammer, mjumbe wa Marekani katika Pembe ya Afrika (picha ya zamani).
Mike Hammer, mjumbe wa Marekani katika Pembe ya Afrika (picha ya zamani). AFP - ORLANDO SIERRA
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia mzozo huu, ambao kwa mara nyingine unatishia kuenea ukanda mzima, jumuiya ya kimataifa inajaribu kuchukuwa hatua. Siku ya Jumamosi Marekani ilituma mjumbe wake kwa Pembe ya Afrika ambaye atakuwa na makao yake mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Wakati wa ziara yake ya awali, mwanzoni mwa mwezi wa Agosti, Mike Hammer alikutana na serikali ya Ethiopia pamoja na waasi wa Tigray wa TPLF. Kambi hizo mbili zilikuwa karibu kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

Mwezi mmoja baadaye, Mike Hammer anawasili Ethiopia katika vita kamili. Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea kwa siku kumi. Makubaliano ya kibinadamu yamesambaratika kabisa. Vyanzo vya misaada ya kibinadamu tayari vinazungumza juu ya maelfu ya waathiriwa katika wiki mbili za mapigano kwenye viunga vya Jimbo la Tigray.

Mjumbe maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika anasafiri hadi Ethiopia kutaka kusitishwa kabisa kwa uhasama. Waziri wake wa Mambo ya Nje, Antony Blinken, sio tu alilaani kuingia kwa Eritrea katika vita, bali pia mashambulizi ya waasi wa TPLF pamoja na mashambulizi ya anga dhidi ya raia yaliyofanywa na jeshi la Ethiopia.

Katika mgogoro huu, washirika wa Magharibi na Umoja wa Afrika hadi sasa wameshindwa kuzileta pamoja pande hizo mbili.

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa pia alikosoa ukosefu wa ufanisi wa Olusegun Obasanjo, mpatanishi aliyechaguliwa na Umoja wa Afrika kutatua mgogoro wa Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.