Pata taarifa kuu

Ethiopia: AU yatiwa wasiwasi na kuzuka tena kwa mapigano

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) amesema Jumatano Agosti 24 kwamba "ana wasiwasi mkubwa" kuhusu kuanza tena kwa mapigano kaskazini mwa Ethiopia kati ya serikali ya shirikisho na waasi kutoka jimbo la Tigray na kutoa wito kwa pande zinazokinzana 'kusitisha mapigano' na kufikiria amani.

Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki, Desemba 18, 2018 wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Austria.
Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki, Desemba 18, 2018 wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Austria. AP - Ronald Zak
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Moussa Faki Mahamat "anatoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa mapigano na anatoa wito kwa wahusika kuanza tena mazungumzo ya kutafuta suluhisho la amani" la mzozo huo ulioanza tangu mwezi Novemba 2020, wakati mapigano yalianza tena Jumatano baada ya miezi mitano. ya amani.

Serikali ya Ethiopia imethibitisha kuwa mapigano haya yameanza tena siku ya Jumatano kaskazini mwa Ethiopia kati ya jeshi la serikali kuu na waasi katika eneo la Tigray, ikishutumu waasi wa Tigray kwa "kuvunja" makubaliano yaliyokuwepo kwa muda wa miezi mitano.

Katika siku za hivi karibuni serikali ya shirikisho na waasi wa Tigrayan wamekuwa wakipaza sauti, kila mmoja akimshutumu mwenzake kwa kujiandaa kuanzisha tena uhasama, licha ya ahadi za mara kwa mara kutoka kwa kila mmoja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita kwa ajili ya mazungumzo ambayo hayajaanza.

Mzozo wa Tigray ulizuka mnamo mwezi wa Novemba 2020, wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alituma jeshi Tigray kuiondoa serikali ya eneo hilo ambayo ilikuwa imepinga mamlaka yake kwa miezi kadhaa na ambayo aliishutumu kushambulia kambi za jeshi la shirikisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.