Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Serikali ya Ethiopia yawatuhumu waasi wa Tigray kuanzisha mapigano mapya

Serikali ya Ethiopia imethibitisha kuwa mapigano haya yameanza tena siku ya Jumatano kaskazini mwa Ethiopia kati ya jeshi la serikali kuu na waasi katika eneo la Tigray, ikishutumu waasi wa Tigray kwa "kuvunja" makubaliano yaliyokuwepo kwa muda wa miezi mitano.

Kifaru cha waasi wa Tigray kilichotelekezwa karibu na Mehoni, Tigray kusini, Ethiopia, tarehe 11 Desemba 2020.
Kifaru cha waasi wa Tigray kilichotelekezwa karibu na Mehoni, Tigray kusini, Ethiopia, tarehe 11 Desemba 2020. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

 

"Kupuuzia matoleo mengi ya amani yaliyowasilishwa na serikali ya Ethiopia", vikosi vya kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) "wameanzisha mashambulizi leo saa 05:00 alfajiri" katika eneo lililoko kusini mwa jimbo la Tigray na "wamevunja makubaliano ya usitishwaji vita", serikali imesema katika taarifa.

"Vikosi vyetu shupavu vya ulinzi na vikosi vyetu vyote vya usalama vinajibu kwa ushindi na kwa njia iliyoratibiwa kwa shambulio hili", imeongeza serikali, ambayo inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa "shinikizo kali" kwa mamlaka ya waasi huko Tigray. Waasi wa Tigray walishutumu kwa mara ya kwanza asubuhi jeshi la shirikisho la Ethiopia kwa kuanzisha "mashambulizi makubwa" dhidi ya ngome zao.

Jimbo la Tigray na maeneo ya mpaka na mikoa jirani ya Amhara na Afar, ambayo baadhi yake ynakaliwa na waasi wa Tigray, kwa kiasi kikubwa yametengwa na nchi nzima na haiwezekani kuthibitisha madai ya kila mmoja kwa kujitegemea au katika uwanja wa mapigano. Mapigano haya ni ya kwanza kwa ukubwa kuripotiwa tangu makubaliano ya amani kuhitimishwa mwishoni mwa mwezi wa Machi na kambi hizo mbili.

Katika siku za hivi karibuni serikali ya shirikisho na waasi wa Tigrayan wamekuwa wakipaza sauti, kila mmoja akimshutumu mwenzake kwa kujiandaa kuanzisha tena uhasama, licha ya ahadi za mara kwa mara kutoka kwa kila mmoja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita kwa ajili ya mazungumzo ambayo hayajaanza.

Mzozo wa Tigray ulizuka mnamo mwezi wa Novemba 2020, wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alituma jeshi Tigray kuiondoa serikali ya eneo hilo ambayo ilikuwa imepinga mamlaka yake kwa miezi kadhaa na ambayo aliishutumu kushambulia kambi za jeshi la shirikisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.