Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa unasema "una wasiwasi" kuhusu haki za binadamu nchini Guinea

Umoja wa Mataifa umemueleza kiongozi wa serikali ya Guinea "wasiwasi wake mkubwa" katika kuhusu hali ya haki za binadamu baada ya vifo vya watu kadhaa wakati wa maandamano ya hivi karibuni na kukamatwa kwa wengine wengi.

Guinea, nchi maskini yenye historia mbaya ya kisiasa, imetawaliwa tangu mwezi Septemba 2021 na jeshi linaloongozwa na Kanali Doumbouya ambaye alimpindua rais wa zamani Alpha Condé na tangu wakati huo aliapishwa kama rais.
Guinea, nchi maskini yenye historia mbaya ya kisiasa, imetawaliwa tangu mwezi Septemba 2021 na jeshi linaloongozwa na Kanali Doumbouya ambaye alimpindua rais wa zamani Alpha Condé na tangu wakati huo aliapishwa kama rais. REUTERS - SALIOU SAMB
Matangazo ya kibiashara

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Michelle Bachelet, amemwandikia barua Kanali Mamady Doumbouya kueleza "wasiwasi wake mkubwa juu ya maendeleo ya hivi karibuni katika hali ya haki za binadamu" nchini mwake. Barua yake, ambayo imekuwa ikisambazwa katika vyombo vya habari vya Guinea tangu Jumapili, imethibitishwa siku ya Jumatatu na wasaidizi wa Bi Bachelet.

Bi Bachelet anakumbusha vifo vilivyosababishwa na matumizi ya nguvu ya vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya Julai 28 na 29. Pia amesema "anatiwa wasiwasi na ripoti za idadi kubwa ya waandamanaji waliokamatwa".

Watu watano waliuawa siku hizi mbili katika vitongoji vya Conakry, na wengine wawili wakati wa siku mpya ya maandamano mnamo Agosti 17 (baada ya barua kutoka kwa Bi Bachelet), kulingana na muungano wa mashirika ya kiraia ambao ulitoa wito wa kuandamana. Utawala wa kijeshi uliamuru mnamo Agosti 6 kufutwa kwa muungano mkuubwa wa upinzani unaodai kutetea ulinzi wa Katiba (FNDC).

"Hatua kama hiyo inajumuisha ukiukaji mkubwa wa haki ya uhuru wa kujumuika na kukusanyika hadharani," ameandika Bi. Bachelet. Ameaomba mamlaka kuchunguza vifo vilivyotokea wakati wa maandamano, kuwaachilia wafungwa na kuidhinishwa tena kwa muungano wa upinzani wa FNDC.

Guinea, nchi maskini yenye historia mbaya ya kisiasa, imetawaliwa tangu mwezi Septemba 2021 na jeshi linaloongozwa na Kanali Doumbouya ambaye alimpindua rais wa zamani Alpha Condé na tangu wakati huo aliapishwa kama rais.

Serikali ya kijeshi imeahidi kurudisha mamlaka kwa raia waliochaguliwa baada ya miaka mitatu. FNDC na waliosalia wa upinzani wanashutumu matumizi ya kimabavu ya madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.