Pata taarifa kuu

Viongozi wa ECOWAS wazijadili Mali, Burkina Faso na Guinea

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, wanakutana jijini Accra nchini Ghana, kujadili hali ya kisiasa nchini Mali, Burkina Faso na Guinea.

Mkutano wa ECOWAS mjini Accra, Ghana.
Mkutano wa ECOWAS mjini Accra, Ghana. © AP - Misper Apawu
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja, baada ya kuwepo kwa mikutano ya wawakilishi wa ECOWAS katika nchi hizo tatu, kujadili hali ya siasa katika nchi hizo ambazo zimeshuhudia mapinduzi ya kijeshi. 

Rais wa Togo Faure Gnassingbé naye amekuwa akijadiliana na wenzake kuhusu hali ya serikali ya mpito ya Mali inayoongozwa na Kanali Asimi Goita kuwa madarakani kwa miaka metano, kabla ya kuandaa uchaguzi. 

Baraza la ushirikiano wa nchi za Kiislamu, nao walituma mjumbe wake katika nchi hizo, mwezi Aprili, kuunga mkono juhudi za mjumbe wa ECOWAS ambaye ni rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan ambaye, amekuwa akijaribu kushawishi nchi hizo kuunda serikali. 

Kwa miezi zaidi ya minne sasa, vikwazo vya kiuchumi vimekewa kwa serikali ya Mali, baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi Agosti mwaka 2020. 

Ripoti zinasema, baada ya kikao cha leo, huenda nchi hizo zikapunguza muda wa serikali za mpito na kurejesha uongozi wa kikatiba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.