Pata taarifa kuu

Mali: Wanajeshi wa Mali na 'Wazungu' wahusika katika mauaji ya raia 33 karibu na Ségou

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, jeshi la Mali na "askari Wazungu" walihusika katika vifo vya raia 33, mwanzoni mwa mwezi Machi, nchini Mali, wakiwemo Wamauritania 29 na Wamali 4, katika mkoa wa Ségou, karibu na mpaka wa Mauritania. 

Picha, iliyopigwa mwishoni mwa mwezi wa Desemba 2021, ikifichua uwepo wa mamluki wa Urusi kutoka kampuni ya Wagner katika eneo la Ségou, lililoko kilomita 200 kaskazini mashariki mwa Bamako, kwenye Mto Niger. Kulingana na waangalizi walio karibu na faili ya Mali, mamluki 200 kutoka kundi la Wagner wanaishi katika eneo hili.
Picha, iliyopigwa mwishoni mwa mwezi wa Desemba 2021, ikifichua uwepo wa mamluki wa Urusi kutoka kampuni ya Wagner katika eneo la Ségou, lililoko kilomita 200 kaskazini mashariki mwa Bamako, kwenye Mto Niger. Kulingana na waangalizi walio karibu na faili ya Mali, mamluki 200 kutoka kundi la Wagner wanaishi katika eneo hili. © Observateur civil anonyme
Matangazo ya kibiashara

Kutoweka kwao kumezua hasira ya mamlaka ya Mauritania ambayo ilfanya uchunguzi wa pamoja kuhusu mkasa huu, na mamlaka ya Bamako. Matokeo, mwanzoni mwa mwezi Agosti, hayajachapishwa. Mali imeendelea kutupilia mbali shutuma hizi dhidi ya jeshi lake.

Ushuhuda uliokusanywa na kundi hilo la wataalamu unaeleza jinsi askari Wazungu walivyowasili katika kijiji cha Robinet El Ataye, kinachotembelewa na wafugaji wa Mali na Mauritania kwa ajili ya kisima chake, jinsi wafugaji hao walivyokusanya wanaume hao, wakiwemo vijana, wakiwafunga mikono nyuma ya migongo yao na kuwafumba macho, huku wanawake na watoto wakiamriwa waende nyumbani na wasiangalie, kisha wakapora nyumba ndani ya majumba.

Kundi la FAMa (Vikosi vya Wanajeshi wa Mali) baadae waliwasili, wakawapiga kwa "fimbo zinazotumiwa na wachungaji"wanaume waliokuwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo", kisha wakawachilia huru waliokuwa na mri mdogo zaidi, na kuwachukua wanaume 33 - 29 Wamauritania na 4 Wamali.

Siku iliyofuata, ndugu wa wahanga waligundua miili yao, umbali wa kilomita 4. Walikuwa wamepigwa risasi na kisha kuchomwa moto.

Mtindo huu wa uporaji na visa vya kupigwa vilijirudi, bila kusababisha vifo, katika vijiji vingine vitano katika eneo hilo tarehe 5 na 6 Machi.

Mashahidi katika ripoti ya Umoja wa Mataifa mara mbili wanataja helikopta iliyobeba askari wenye Wazungu. Mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner wanashukiwa mara kwa mara kwa dhuluma dhidi ya raia nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.