Pata taarifa kuu

Mali: UN yashutumu wanajeshi wa Mali na 'Wazungu' kwa kuhusika katika mauaji ya raia 33

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema, katika ripoti ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi siku ya Ijumaa, kwamba wanajeshi wa Mali na "Wazungu" walihusika katika mauaji ya raia 33 nchini Mali mnamo Machi 5. Watu hawa, wengi wao wakiwa Wamauritania, walikuwa wametoweka ghafla, katika mazingira yasiyoeleweka.

Bamako inakanusha uwepo wa mamluki hawa, ikimaanisha uwepo wa "wakufunzi", huku Moscow ikidai kuwa haina uhusiano wowote na kampuni hii iliyopo Mali kwa "msingi wa kibiashara".
Bamako inakanusha uwepo wa mamluki hawa, ikimaanisha uwepo wa "wakufunzi", huku Moscow ikidai kuwa haina uhusiano wowote na kampuni hii iliyopo Mali kwa "msingi wa kibiashara". © @ RFI Mandenkan
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo ilizua taharuki katika pande zote za mpaka. Jeshi la Mali na "askari Wazungu" wanahusika katika vifo vyaraia 33 mapema mwezi Machi nchini Mali, karibu na mpaka wa Mauritania, wakiwemo raia 29 wa Mauritania na 4 wa Mali, kulingana na ripoti ya wataalam iliyoagizwa na Umoja wa Mataifa Ijumaa, Agosti 5.

Miili ya raia hawa ilipatikana kilomita chache kutoka kijiji cha Robinet El Ataye katika mkoa wa Ségou, ambapo "askari Wazungu", wa kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, kulingana na mwanadiplomasia huko New York, na wanajeshi wa Mali, siku moja kabla, Machi 5, waliwakamata, kuwafunga, kuwapiga na kuwakama watu hao 33, inasema ripoti hii ya Kundi la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mali ambayo ilitumwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Kutoweka kwa raia hawa, katika mazingira yasiyoeleweka wakati huo, mnamo Machi 5 huko Robinet El Ataye, kulizua taharuki nchini Mali na Mauritania.

Bamako yakanusha uwepo wa mamluki

Nouakchott ilikuwa imelishutumu jeshi la Mali kwa "vitendo vya uhalifu vya mara kwa mara" dhidi ya raia wa Mauritania katika eneo hili la mpaka. Bamako ilisema kwamba hakuna chochote kilichotilia shaka jeshi lake.

Nchi hizo mbili zilikuwa zimefungua uchunguzi wa pamoja, ambao matokeo yake hayakuwa yamechapishwa mapema mwezi Agosti.

Ripoti ya Kundi la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mali, ambayo ilitumwa kwa Baraza la Usalama mwishoni mwa Julai na ambayo shirika la habari la AFP liliweza kuisoma Ijumaa, inatoa shaka kwa mazingira ya kutatanisha kuhusiana na vifo vya raia hawa 33 na kulishtumu jeshi la Mali na "askari Wazungu"kuhusika.

Pande hizi mbili ni sehemu, kulingana na mwanadiplomasia wa New York ambaye ameliambia shirika la habari la AFP, wa wanamgambo wa kundi la Wagner waliotumwa kusaidia wanajeshi wa Mali tangu mwezi Januari. Bamako inakanusha uwepo wa mamluki hawa, ikimaanisha uwepo wa "wakufunzi", huku Moscow ikidai kuwa haina uhusiano wowote na kampuni hii iliyopo Mali kwa "msingi wa kibiashara".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.