Pata taarifa kuu

Chad: Kifo cha Idriss Déby, rais mbabe wa kivita

Mwaka mmoja aas umepita tangu rais wa Idriss Déby afariki dunia katika mazingira ya kutatanisha, katikati mwa mashambulizi ya waasi wa FACT, nchini Chad, na Baraza la Mpito la kijeshi likaanzishwa. Siku chache kabla ya maadhimisho haya ya kwanza, RFI inakupa uchunguzi wa pamoja katika vipindi vinne kuhusu mazingira ya kifo cha rais wa Chad, na kuhusu hali ya kipindi cha mpito leo, kulingana na shuhuda nyingi.

Rais wa zamani wa Chad Idriss Déby.
Rais wa zamani wa Chad Idriss Déby. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Toleo rasmi lililozua utata, uchunguzi ambao bado haujahitimishwa... Nvigumu kwa N'Djamena, kusema kuhusiana na dhana kuhusu mazingira ya kifo cha Idriss Déby...

"Inaweza kuonekana kuwa ni jambo lisiloeleweka kusikia kwamba rais wa nchi, katika wakati wetu, aliuawa vitani. Hata hivyo, ni ukweli ulio sahihi" amesema mmoja wa washauri wake wa zamani ..." Hii ni mwa vitu ambavyo Déby alitaka, alirejelea mara nyingi hali hii kwa watu wake"...

"Kama angeliuawa na mtu, mtu huyo naye angeuawa, kungekuwa na ulipizaji kisasi, hali hii ingelizua mtafaruku" ameongeza ofisa mmoja ambaye mara moja amepuuzia mbali nadharia yoyote mbadala...

Hata leo, kwa undani, mazingira ya kifo cha Marshal katika vita vya vya Zigueï bado ni ya kushangaza ...

Majibizano ya risasi yalikuwa makali na,  hivyo Idriss Déby kupigwa risasi.

Wengine wanadai kuwa mapigano hayo mabaya yalifanyika Jumapili jioni Aprili 18, wengine Jumatatu Aprili 19 alfajiri ...

Je waasi wa FACT walijua alikuwa katika eneo hilo la mapigano? Waasi hao waliweza kumtafuta na kumpiga risasi? kiongozi wake, Mahamat Mahdi Ali ameeleza hili kwa kirefu katika uchunguzi wetu...

Jambo lingine la kutokuwa na uhakika: alikufa kwa risasi, au kwa bomu? hata hivyo, hakuna uchunguzi wa maiti uliofanyika.

Huku wanajeshi wake wakihakikisha ushindi wa kijeshi, rais wa nchi aliondoka uwanja wa vita, akisafirishwa kwa helikopta, akiwa amejeruhiwa vibaya...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.