Pata taarifa kuu
CHAD-MAZUNGUMZO

Chad: mazungumzo kati ya utawala wa kijeshi na waasi kuanza Jumapili huko Doha

Wanajeshi walio madarakani nchini Chad tangu kifo cha Rais Idriss Déby, aliyeuawa miezi kumi iliyopita akiwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya waasi, wataanza mazungumzo yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu nchini Qatar siku ya Jumapili na makundi mengi ya waasi.

Rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi Mahamat Idriss Déby wakati wa mkutano nchini Sudan, mjini Khartoum mnamo Agosti 29, 2021.
Rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi Mahamat Idriss Déby wakati wa mkutano nchini Sudan, mjini Khartoum mnamo Agosti 29, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Mazungumzo haya ya kabla ya Doha" yaliyoahidiwa kwa miezi mingi na ambayo yalipangwa kufanyika Februari 27, yaliahirishwa dakika za mwisho hadi Machi 13.

"Qatar itakuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani ya Chad Jumapili Machi 13," Dk. Mutlaq Al-Qahtani, mwakilishi maalum wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar wa Kupambana na Ugaidi na Upatanishi katika utatuzi wa migogoro, ametangaza huko Doha.

Lakini sherehe za ufunguzi zitafanyika bila sehemu kubwa ya viongozi 84 na makada wa makundi 44 yenye silaha walioalikwa, kulingana na mjumbe wa upatanishi wa Chad, ambao bado hawajaweza kuondoka mafichoni huko Libya, Sudan au mbali zaidi, tena, kwa sababu hati zao za kusafiri hazikufika kwa wakati.

Kiongozi wa waasi aliyewasiliana kwa njia ya simu amelihakikishia shirika la habari la AFP kwamba waandaaji walimwambia "kwamba kuwepo kwenye ufunguzi sio wajibu na kwamba kulikuwa na ucheleweshwaji fulani".

Lengo lililotajwa na Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, 38, mtoto wa hayati Idriss Idriss Déby Itno na aliyejitangaza kuwa Rais wa Jamhuri mnamo Aprili 20, 2021 akiwa akiongoza majenerali 15, alisema ni kuzungumza na waasi "wote", ikiwa ni pamoja na muungano wa waasi wenye nguvu zaidi,  wa FACT, unaotuhumiwa kumuua baba yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.