Pata taarifa kuu
CHAD-MAZUNGUMZO

Chad: Mamlaka yatetea kuahirishwa kwa mazungumzo ya kitaifa

Baada ya kuahirishwa kwa mazungumzo ya kitaifa jumuishi hadi Mei 10, 2022 badala ya Februari 15, serikali ya Chad imetaka kuelezea washirika wake kwamba inajaribu kufanya mambo sawa na ingependa kuwategemea.

Cherif Mahamat Zène, Waziri wa Mmambo ya Nje wa Chad.
Cherif Mahamat Zène, Waziri wa Mmambo ya Nje wa Chad. Getty Images via AFP - ANDREW BURTON
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad amejaribu kwaelezea mabalozi wanaowakisha nchi zao nchini Chad sababu za kuahirishwa kwa mazungumzo ya kitaifa ya umoja, mchakato ambao utawezesha Chad kujenga upya mfumo wa kisiasa.

Ikiwa mazungumzo ya kitaifa yataahirishwa, ni kuruhusu Qatar, baada ya kujitolea kuandaa mazungumzo ya awali ya viongozi wa makundi ya wanasiasa walioamua kushika silaha , kuandaa ushiriki wao vyema.

"Kuahirishwa huku kuna dhamira pekee ya mafanikio ya kabla ya mazungumzo na ushiriki wa pamoja wa wahusika wote wanaohusika katika mazungumzo ya kitaifa ya umoja", amebaini Waziri wa Mmbo ya Nje wa Chad, Chérif Mahamat Zène.

Lakini ili kukamilisha kipindi cha mpito, serikali inahitaji mshikamano wa kimataifa, amekumbusha Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad. "Serikali inategemea uelewa wenu na uungwaji wenu mkono kwa mshikamano ili kuendeleza kipindi cha mpito kwa mafanikio hadi mwisho wa mua wake. Katika suala hili, ni muhimu kusisitiza kwamba uhamasishaji wa rasilimali muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa yaliyokubaliwa bado yanaendelea kutia wasiwasi mkubwa serikali ya mpito."

Uchaguzi umepangwa kabla ya mwisho wa mwaka

Mshikamano ambao hata hivyo unasalia kuwa na masharti ya ahadi za uwazi wa kidemokrasia. Katika suala hili, viongozi wa mapinduzi pia wametaka kuhakikisha: Chérif Mahamat Zène amethibitisha kwamba kuahirishwa kwa mazungumzo "hautazuia" kufanyika kwa uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka.

Jambo muhimu kwa Umoja wa Afrika. Kwa sababu ikiwa hata hivyo ingehitaji kipindi cha mpito cha miezi 18, jumuiya hii inaona kuahirishwa huku kuwa kunakubalika, mradi tu mabadiliko haya yasizidi mwisho wa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.