Pata taarifa kuu

Chad: Mazungumzo ya kitaifa ya Februari 15 yaahirishwa kwa miezi mitatu

Serikali inaelezea kuahirishwa huku kunatokana na nia njema ya kuhusisha masuala muhimu zaidi katika mazungumzo haya. Lengo la mazungumzo haya ni kuamua juu ya mwisho wa kipindi cha mpito kilichoanza baada ya kifo cha rais Idriss Déby Itno.

Ikulu ya rais wa Chad, inapatikana katika eneo la Djambel Bahr, Ndjamena, Mei 2021.
Ikulu ya rais wa Chad, inapatikana katika eneo la Djambel Bahr, Ndjamena, Mei 2021. © David Baché
Matangazo ya kibiashara

Ushiriki wa wanasiasa walioamua kushika silaha dhidi ya serikali katika mkutano huu, ambao mahitimisho yake yanapaswa kuamua kuendelea kwa mchakato wa kisiasa nchini Chad, ndio chanzo cha kuahirishwa kwa mazungumzo hayo.

"Inaonekana kwamba, katika maandalizi, nchi mwenyeji, Qatar hasa, baada ya kugundua kutawanyika kwa wanasiasa walioamua kushika silaha dhidi ya serikali katika mataifa mbalimbali zilizokatika vita, wengi wao hawana hati ya kusafiri. Chad wanapaswa kuwatafutia hati za kusafiria. Na masuala haya yote ya vifaa yalisababisha nchi mwenyeji kupendekeza kuleta pamoja wanasiasa walioamua kushika bunduki dhidi ya serikali, kuanzia Februari 27, 2022”, amebaini Waziri Mkuu wa kipindi cha mpito, Pahimi Padacké Albert.

Baada ya mazungumzo ya awali ya mjini Doha, ambayo yanapaswa kudumu wiki mbili, Machi 10 mahitimisho yatawasilishwa kwa kamati ya maandalizi ya mazungumzo jumuishi ya kitaifa. Ripoti ambayo itaunganishwa katika ile ya midahalo ya awali iliyoandaliwa katika majimbo tofauti na ambayo itatakiwa kutoa muhtasari wa kile wananchi wa Chad wanatarajia kutoka kwa nchi yao katika siku zijazo.

Ni baada ya zoezi hili ambapo Waziri Mkuu wa Mpito ataitisha mazungumzo ya kitaifa ambayo yametangazwa kufanyika Mei 10, 2022.

Shida kubwa ni ajenda gani ya mazungumzo? Ni jambo la kimantiki tu kwamba tunaweza kukubaliana juu ya mambo ya ndani na kufikia mazungumzo kabla ya kuyaanza, " amesema wakili Max Loalngar, msemaji wa muungano wa vyama vya siasa na vyama vya kiraia Wakit TAma, akihojiwa na Bineta Diagne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.