Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Mazungumzo ya kitaifa ya Chad yaahirishwa hadi Februari 15

Kiongozi wa utawala wa kijeshi, Jenerali Mahamat Idriss Deby, katika ujumbe wake wa jadi kwa taifa ametangaza tarehe ya kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa  Februari 15.

Max Loalngar (katikati), kiongozi wa uratibu wa vitendo vya raia la vuguvugu la Wakit Tamma, Barka Michel na Citak Yombatinan, katika mkutano na waandishi wa habari Juni 8, huko Ndjamena.
Max Loalngar (katikati), kiongozi wa uratibu wa vitendo vya raia la vuguvugu la Wakit Tamma, Barka Michel na Citak Yombatinan, katika mkutano na waandishi wa habari Juni 8, huko Ndjamena. AFP - DJIMET WICHE
Matangazo ya kibiashara

Kinyume na matarajio yote, rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi, Jenerali Mahamat Idriss Deby, ametangaza kuwa mazungumzo ya kitaifa nchini Chad yatafanyika Februari 15.

Hata ivyo, Baraza la Mawaziri lilikuwa limepitisha kwamba mazungumzo hayo ya kisiasa yangelifanyika kati yamwezi  Novemba na Desemba mwaka wa 2021.

Mazungumzo hayo, ambayo yanapaswa kuwa bila miiko, yanapaswa kuwezesha kutengenezwa kwa Katiba mpya ambayo baadaye itapitishwa kwa kura ya maoni kwa wananchi wote wa Chad. Inapaswa pia kufuata uchaguzi mkuu ulio huru, wa uwazi na wa kidemokrasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.