Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Chad: Mwanajeshi mmoja atoweka baada ya tukio kwenye mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mwanajeshi wa Chad ametoweka tangu Jumapili, Desemba 12 kufuatia mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi. Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama vya Chad, hili lilikuwa tukio lililosababishwa na mapigano kati ya majeshi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ndani ya nchi hiyo na kusambaa hadi kwenye mpaka na Chad.

Wanajeshi wa Chad wakiwa nje ya mahakama ya Ndjamena (picha ya kumbukumbu 2007).
Wanajeshi wa Chad wakiwa nje ya mahakama ya Ndjamena (picha ya kumbukumbu 2007). Thomas SAMSON/Gamma-Rapho via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yametokea kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Safu ya wanajeshi wa Jmahuri ya Afrika ya Kati, wakiungwa mkono na wakufunzi wa kampuni ya Wagner kutoka Urusi, walishambulia Jumapili, Desemba 12 ngome ya waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokuwa wakirudi nyuma kuelekea Chad.

Katika operesheni hiyo, kituo cha jeshi la Chad kusini mwa Moïssala, kwenye ukingo wa mpaka wa Jamahuri ya Afrika ya Kati, kilishambuliwa. Kulikuwa na urushianaji risasi kati ya wanajeshi wa serikali na waasi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati na, kulingana na vyanzo rasmi kutoka Ndjamena, mwanajeshi wa Chad hajulikani aliko kufikia sasa. Hakuna mtu aliyevuka mpaka wa Chad, amesema msemaji wa serikali ya Chad Abderahman Koulamallah.

Hii ni mara ya pili tangu mwezi Mei kwa tukio kama hilo kukumba vikosi vya Chad. Shambulio la jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati dhidi ya waasi kutoka nchi hiyo tayari lilisababisha vifo vya wanajeshi sita wa Chad mnamo Mei 30 baada ya kuvuka mpaka na kuingia nchini Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.