Pata taarifa kuu

Mpinzani wa Chad Tom Erdimi yuko hai, yasema familia yake

Tom Erdimi yuko hai. Kaka yake pacha, Timane Erdimi, anathibitisha hili kwa RFI. Mpwa ambaye anamwamini na ambaye aliandamana na Rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi (TMC) Mahamat Idriss Déby hadi Misri, aliweza kumtembelea mpinzani wa Chad katika gereza la Cairo ambako anazuiliwa. Familia ilikuwa haina habari tangu mwishoni mwa mwa 2020.

Tom Erdimi, katika mkutano wa UNESCO mwaka 1992.
Tom Erdimi, katika mkutano wa UNESCO mwaka 1992. © Derdimi/creative commons
Matangazo ya kibiashara

Mpwa wetu alimpata akiwa salama na mwenye afya njema. Alikaa naye kwa muda wa saa mbili (...) Alituambia kuwa amepata maelekezo ya kufuatilia faili hilo hadi kuachiliwa kwake moja kwa moja.

Tom Erdimi, ambaye alikuwa mpwa na mkurugenzi wa kwanza katika ofisi ya Idriss Deby Itno lakini pia mratibu wa zamani wa mradi wa mafuta, alitoweka tangu mwishonimwa mwaka 2020. Aliachana na serikali ya mjomba wake kabla ya kujiunga na Muungano wa Majeshi ya Upinzani (UFR), kundi la waasi linaloongozwa na pacha wake Timane Erdimi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.