Pata taarifa kuu
CHAD-USHIRIKIANO

Misri na Chad kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali

Mkuu wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Chad, Mahamat Idriss Déby, alifanya ziara ya siku mbili nchini Misri ambapo alipokelewa na Rais Abdel Fattah al-Sisi. Ujumbe ulioandamana na Bw. Déby ulikutana na maafisa kadhaa wakuu wa Misri.

Rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi Mahamat Idriss Déby wakati wa mkutano nchini Sudan, mjini Khartoum, Agosti 29, 2021.
Rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi Mahamat Idriss Déby wakati wa mkutano nchini Sudan, mjini Khartoum, Agosti 29, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa za pande zote mbili, marais hao wa Misri na Chad wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika ngazi za kisiasa, kiuchumi na kijeshi. Rais wa Misri alionyesha wazi kuwa Cairo itaiunga mkono Ndjamena wakati wa kipindi cha mpito kuelekea demokrasia. Hata hivyo, mada ambayo ilijadiliwa zaidi na wawili hao ni hali ya wasiwasi nchini Libya na athari ambayo inaweza kusababisha nchini Chad na Misri.

Wakati huo huo, mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa nchi hizo mbili wamekubaliana kuzindua upya mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kidiplomasia na pia katika ngazi ya kubadilishana taarifa za kijeshi. Ushirikiano katika ugavi na mafunzo pia ulikuwa moja ya mada ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili. Misri na Chad zina uhusiano mzuri tangu miaka ya 1980. Cairo ilikuwa ikiunga mkono Ndjamena katika vita vyake dhidi ya Libya ya Kanali Gaddafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.