Pata taarifa kuu

Chad: Vipi kuhusu mazungumzo ya awali ya Doha baada ya Goukouni Weddeye kutengwa

Maswali kuhusu mazungumzo ya awali yaliyopangwa kuanzia Jumapili huko Doha, Qatar, na makundi ya kisiasa na wapiganaji nchini Chad. Hadi wakati huo akisimamia mazungumzo na makundi haya, Rais wa zamani Goukouni Weddeye amepoteza imani kwa mamlaka ya Ndjamena.

Rais wa zamani wa Chad Goukouni Weddeye.
Rais wa zamani wa Chad Goukouni Weddeye. ( Photo : Laurent Correau )
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutengwa kwa Goukouni Weddeye, mkutano ambao unatarajia kufungua njia ya kuunganishwa kwa makundi yenye silaha ndani ya mazungumzo ya kitaifa ya siku zijazo hautishiwi. Zaidi ya hayo, waziri wa mambo ya nje wa Chad alitarajiwa kuondoka Alhamisi asubuhi kwenda Doha na kuendeleza majadiliano yaliyoanzishwa na Qatar, kama mpatanishi.

Kulingana na chanzo cha serikali, inaelezwa kuwa tayari zimepita wiki kadhaa tangu Cherif Mahamat Zene achukue jukumu la maandalizi ya mkutano huu na kwamba ni jambo la kimantiki kwamba achukue nafasi ya rais wa zamani Goukouni Weddeye, ambaye kazi yake ya kuleta wanasiasa na wapiganaji kwenye meza ya mazungumzo, imekamilika. Hata hivyo Goukouni Weddeye ameelezea mshangao wake aliposikia aliondolewa kwenye nafasi hiyo.

Qatar iliomba mazungumzo hayo yafanywe na mamlaka ya serikali. Hivyo kuanzishwa kwa "kamati mpya maalum", inayoundwa na wajumbe 25, inayoongozwa na waziri wa mambo ya nje.

"Goukouni alikuwa mtu sahihi"

Kuhusu kubadilishwa kwa mpatanishi, makundi ya kisiasa na wapiganaji yamepokea shingo upande kwa sababu msimamo wa rais huyo wa zamani, anayeheshimiwa na wote, ulikuwa umewezesha kuendeleza majadiliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.