Pata taarifa kuu

Chad: UFR yajibu baada ya mabishano yaliyosababishwa na kauli ya Erdimi kuhusu Wagner

Nchini Chad, vuguvugu la kisiasa na kijeshi la UFR la Timana Erdimi hatimaye limejibu kuhusiana na matamshi ya Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya Chad, Abderaman Koulamallah.

Kiongozi wa UFR Timan Erdimi mwaka 2009 huko Darfur.
Kiongozi wa UFR Timan Erdimi mwaka 2009 huko Darfur. © GUILLAUME LAVALEE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Abderaman Koulamallah alikuwa ametangaza kwamba Timan Erdimi amejiondoa kwenye mazungumzo ya awali ya Doha, baada ya maneneo yake kuvuja kwenye mitandao ya kijamii kufuatia sauti yake ambapo alisikika akimwambia waziri wa zamani mshauri wa rais wa Afrika ya Kati, kuhusu nia yake ya kutaka kushirikiana na kundi la la wanamgambo kutoka Urusi la Wagner. Msemaji wa UFR amejibu.

Katika sauti hiyo iliyovuja na kuthibitishwa na vyanzo kadhaa, Timan Erdimi, kiongozi wa UFR, anazungumza na waziri wa zamani mshauri maalum wa rais wa Afrika ya Kati, Aboulkassim Algoni Tidjani. Kiongozi huyo wa waasi wa Chad anasikika akielezea nia yake ya kushawishi kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, wanaofanya kazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na serikali ya nchi hii, kumsaidia "kumuondoa mamlakani rais wa Kamati ya Mpito ya Kijeshi" nchini Chad, Mahamat Idriss. Deby.

"Ikiwa Timan Erdimi ana uwezo wa kwenda kufanya mapatano na shetani kuja na kuhatarisha usalama wa nchi, ni jambo zito sana. Hatutakubali kwamba mtu huyu anayepanga kuingia vitani wakati ambapo watu wanataka kufanya amani anaweza kuhudhuria mashauriano ya kabla ya mazungumzo,” msemaji wa serikali Abderaman Koulamallah alipinga.

Kundi la waasi la UFR, kupitia msemaji wake Youssouf Hamid, linasema kuwa linasikitishwa na kilichotokea, huku likikumbusha kwamba halina makubaliano ya kusitisha mapigano na serikali ya kijeshi inayotawala.

"Tunasikitishwa na kitendo hiki, ambacho kinakuja wakati UFR iko tayari kuendelea, pamoja na makundi mengine yote ya kisiasa na kijeshi, mchakato uliosababishwa na CNT, kufikia mazungumzo jumuishi ya kitaifa.

Hata hivyo, ninawakumbusha kwamba UFR haijatia saini makubaliano na Baraza la Kijeshi la Mpito, isipokuwa kwa kukubali kuhudhuria mazungumzo ya awali, kama vile makundi mengine ya kisiasa na kijeshi yaliyo alikwa kuhudhuria katika mazungumzo hayo.

Upande wetu, tunasikitishwa na hali hii ambayo ni sera ya ubaguzi, kwa vile tuko katika awamu ya mpito. Kutengwa ni jambo ambalo halifai kwa mtu yeyote na husababisha migogoro tu…”

RFI: msemaji wa serikali alisisitiza zaidi kwa kiongozi wa UFR, Timan Erdimi, na sio kwa kundi lenyewe ...

"Tunazungumza kuhusu UFR kama muungano. Hatuzungumzii mtu. Ikiwa Bw Koulamallah alisema hivyo... hilo ni tatizo lake. Lakini tumejitolea kwa mazungumzo ya kitaifa, hasa yale ya kabla ya mazungumzo yatakayofanyika Doha”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.