Pata taarifa kuu

Bangui yakataa mawasiliano yoyote na kiongozi wa waasi wa Chad Timan Erdimi

Nchini Chad, kuna wasiwasi baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa mazungumzo ya simu yaliyorekodiwa kati ya kiongozi wa kundi lenye silaha la Chad na waziri wa zamani wa Afrika ya Kati kuhusu kundi la Wagner.

Kiongozi wa kundi la waasi la UFR Timan Erdimi mwaka 2009 huko Darfur.
Kiongozi wa kundi la waasi la UFR Timan Erdimi mwaka 2009 huko Darfur. © GUILLAUME LAVALEE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumatano alasiri, wabunge wa Chad walimtaka Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, kumuitisha balozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aje kueleza uhusiano kati ya Bangui na Timan Erdimi.

Katika sauti hiyo iliyorekodiwa, iliothibitishwa na vyanzo kadhaa, Timan Erdimi, kiongozi wa kundi la waasi la UFR, anasikika akizungumza na waziri wa zamani mshauri maalum wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Aboulkassim Algoni Tidjani. Kiongozi wa waasi wa Chad anasikika akielezea nia yake ya kushawishi kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, wanaofanya kazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na serikali ya nchi hii, kumsaidia "kumuondoa mamlakani rais wa Kamati ya Mpito ya Kijeshi", Mahamat Idriss Deby.

Kwa upande wake msemaji wa ikulu ya rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Albert Yaloké Mokpeme, amefutilia mbali kuhusika kwa aina yoyote kwa Bangui katika mpango huo. Abdoulkassim Algoni Tidjani ni muasi wa zamani, anasema, ambaye alikuwa amejumuishwa katika serikali kama sehemu ya mapatano ya amani ya Khartoum. Miezi kadhaa baada y kuteuliwa kama mshauri maalum wa rais, aliondolewa majukumu yake kwa kwa sheria ya rais mwaka mmoja uliopita, mnamo Februari 19, 2021.

"Hatuhusiki kwa karibu au kwa mbali" na mazungumzo haya, amebainisha msemaji wa Ikulu ya rais ambaye ameongeza: "Ndjamena isiwe na wasiwasi kuhusu kuhusika kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mpango ho potovu. "

Afisa mwingine wa Afrika ya Kati aliyetajwa katika mazungumzo haya kati ya Timan Erdimi na Aboulkassim Algoni Tidjani, ni Waziri wa Mifugo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Hassan Bouba. Anachukuliwa kama mtu muhimu kwa kukutanisha kiongozi wa waasi wa Chad na kundi la mamluki la Wagner. Akihojiwa na RFI, waziri huyu ameelezea mshangao wake. "Ninawasiliana mara kwa mara na Warusi kama sehemu ya kazi yangu kuwashawishi wanachama wa muungano wa waasi, CPC, kuweka silaha chini. Labda ndio maana nilitajwa,” amejibu. "Ninafanya kazi kwa ajili ya amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na si kwa ajili ya kuivuruga Chad. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.