Pata taarifa kuu
CHAD

Watu kadhaa waandamana dhidi ya utawala wa kijeshi Chad

Watu mia kadhaa wameandamana Jumamosi hii huko N'Djamena dhidi ya utawala wa kijeshi ambao unaongoza Chad tangu kifo cha Idriss Déby Itno, wakizungukwa na maafisa wengi wa polisi, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Waandamanaji wanaoshiriki maandamano haya, yanayofanyika mara kwa mara tangu kifo cha rais wa zamani Idriss Déby Itno mnamo mwezi Aprili, pia wanapinga mwenendo wa Ufaransa, iliyotawala Chad katika enzi za ukoloni, ambayo inastumiwa na baadhi ya vyama vya upinzani kuunga mkono utawala mpya.
Waandamanaji wanaoshiriki maandamano haya, yanayofanyika mara kwa mara tangu kifo cha rais wa zamani Idriss Déby Itno mnamo mwezi Aprili, pia wanapinga mwenendo wa Ufaransa, iliyotawala Chad katika enzi za ukoloni, ambayo inastumiwa na baadhi ya vyama vya upinzani kuunga mkono utawala mpya. © Madjiasra Nako/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kiraia yameitisha maandamano dhidi ya sheria za Baraza la Jeshi la Mpito (CMT), linaloongozwa na mtoto wa Idriss Déby, Mahamat Idriss Déby Itno.

Maandamano haya, yanayofanyika mara kwa mara tangu kifo cha rais wa zamani Idriss Déby Itno mnamo mwezi Aprili, pia yanashutumu mwenendo wa Ufaransa, iliyotawala Chada katika enzi za ukoloni, ambayo inastumiwa na baadhi ya vyama vya upinzani kuunga mkono utawala mpya.

"Chad sio nchi ya kifalme", ​​"Tunapinga Ufaransa kuunga mkono mfumo utawala wa baba na mtoto", ni maneneo ambayo yameandikwa kwenye mabango ya waandamanaji.

Maandamano hayo yalikuwa yameidhinishwa na mamlaka. Idadi kubwa ya maafisa wa poisi walonekana wakitoa ulinzi wa waandamanaji, huku maandamano yakifanyika kwa amani, kulingana na mwandishi wa habari wa AFP.

Succès Masra, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa Déby na mwanzilishi wa vuguvugu la kisiasa Les Transformateurs, ameshiriki kwa mara ya kwanza katika moja ya maandamano haya tangu kifo cha Rais-Marshal Déby.

"Tnakumbuka ndugu zetu waliouawa, hatupaswi kukata tamaa," amewaambia waandishi wa habari. Aprili 27, watu sita waliuawa huko N'Djamena na kusini mwa Chad, kulingana na mamlaka, tisa kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali, wakati wa maandamano yaliyopigwa marufuku.

"Tunaandamana leo kudai marekebisho ya sheria inayosimamia kipindi cha mpito na kukemea sheria zinazounda kamati za mazungumzo zisizojumuisha",  Max Loalngar, msemaji wa Wakit Tamma, muungano wa upinzani amebaini, kwa upande wake.

Tangu kutangazwa kifo cha Rais Déby mnamo Aprili 20, Mahamat Idriss Déby Itno, 37, aliahidi uchaguzi "huru na wa kidemokrasia" kufuatia mazungumzo ya kitaifa yanayolenga kupatanisha raia wote wa Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.