Pata taarifa kuu
CHAD

Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré aaga dunia

Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré amefariki dunia Jumanne, Agosti 24, akiwa na umri wa miaka 79. Alilazwa hospitalini mwishoni mwa mwezi Agosti huko Dakar, nchini Senegal - alikokuwa akitumikia kifungo chake cha maisha - baada ya kuambukizwa virusi vya Covid-19.

Hissène Habré amezungukwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa na jaji, Julai 2, 2013 huko Dakar.
Hissène Habré amezungukwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa na jaji, Julai 2, 2013 huko Dakar. AFP/Stringer
Matangazo ya kibiashara

"Bwana Hissène Habré amefariki dunia. Hii ni habari ya kusikitisha sana kwa familia yake, kwa raia wengi wa Chad, na tunahuzunishwa na kifo chake. Hissène Habré alitawala Chad, hata kama hatufarahishwi na namna alivyotawala Chad, kwa kifo chake, tunapaswa kuhuzunishwa”, Abderaman Koulamallah, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya Chad ameiambia RFI.

Uvumi wa kifo cha rais wa zamani wa Chad ulianza jioni ya Jumatatu, Agosti 23 na taarifa kutoka kwa mke wa Hissène Habré, Fatimé Raymonne Habre, ambaye alibaini kuwa rais huyo wa zamani alikuwa ameambukizwa virusi vya Covid-19. Lakini kwa upande wake, mamlaka ya magereza nchini Senegal ilisema kwamba hakuna kesi ya Covid-19 iliyorekodiwa katika jela alikokuwa amezuiliwa, ameripoti mwandishi wetu huko Dakar, Théa Olivier.

Kwa hivyo aliambukizwa wakati alipokuwa katika kliniki ya kibinafsi kabla ya kutibiwa katika hospitali ya umma, kulingana na mkewe. Habari ambayo imethibitishwa na Waziri wa Sheria wa Senegal.

Hissène Habré alikuwa kizuizini "huko Cap Manuel, siku chache zilizopita," Waziri Malick Sall ameiambia RFI. Mkewe ndiye ambaye alizungumza kuhusu hali yake ya afya: "Kwa hivyo aliomba ahamishwe kwa kliniki ya daraja la kwanza huko Dakar," ameongeza Waziri Malick Sall.

Habre ambaye serikali yake ilituhumiwa kwa mauaji ya maelfu ya watu na kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi kuhukumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na mahakama ya Afrika baada ya kuishi uhamishoni Senegal kwa miongo mingi alifariki katika hospitali moja ya mjini Dakar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.