Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Makumi ya watalii wa Urusi wakamatwa eneo la Sahel upande wa Chad

Watalii waurusi na mmoja raia wa Lithuania waliokamatwa zaidi ya wiki moja iliyopita katika eneo la Sahara lililoko upande wa Chad, karibu na Faya-Largeau kaskazini mwa nchi hiyo wamefikishwa Ndjamena. Watalii hao wamesafirishwa hadi Ndjamena, na sasa wamelekwa katika hoteli ya kifahari, wakisubiri kumalizika uchunguzi kubaini sababu za wao kupatikana katika eneo maalum linaloshuhudia mapigano ya mara kwa mara dhidi ya makundi ya magaidi.

Askari wa jeshi la Chad akifanya mazoezi katika eneo hilo la Faya-Largeau, kaskazini mwa Chad.
Askari wa jeshi la Chad akifanya mazoezi katika eneo hilo la Faya-Largeau, kaskazini mwa Chad. © Sgt. Derek Hamilton (US Army) / Creative Commons
Matangazo ya kibiashara

Kundi hili la watalii wasiopungua kumi, miongoni mwao tisa kutoka Urusi na mmoja raia wa Lithuania, yadaiwa waliwasili katika eneo hilo mei 25 wakitokea nchi jirani ya Cameroun 5, kabla ya kuelekea nchini Chadi wakitumia magari yenye uzoefu yanayotumiwa na wanajeshi kuelekea maeneo ya Sahara.

Vyanzo vya kiusalama vinasema watalii hawa walikamatwa karibu na mji wa Faya-Largeau kaskazini mwa Chad, zaidi ya wiki moja iliyopita.

Maafisa wa usalama wamekiri kuwanyanganya pasi zao za kusafiria, simu zao za mkononi, kompyuta mpakato na dira walizozitumia pamoja na mitambo yao ya setlite.

Watu hawa waliosafirishwa mwanzoni mwa juma hili, hadi jijini Ndjamena, ambapo waliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani katika hoteli moja ya kifahari kupisha uchunguzi kubaini ni kwanini walikutwa katika eneo lenye shughuli nyingi za kijeshi, eneo ambalo jeshi la Chad limekuwa lipambana na makundi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.