Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Upinzani wagawanyika baada ya Mahamat Idriss Déby kuutaka kurejea nchini

Nchini Chad, Rais Mahamat Idriss Déby amekuwa akiyatolea wito  makundi yenye silaha mara kadhaa kujiunga katika mchakato wa amani na ujenzi wa taifa.

N'Djamena, mji mkuu wa Chad.
N'Djamena, mji mkuu wa Chad. © David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa kuamkia sikukuu ya kitaifa, ametoa tena "wito kwa makundi yenye silaha kutafakari tena msimamo wao na kutuona kwa lengo la kulijenga taifa". Wito ulioitikiwa na baadhi ya makundi yenye silaha na baadhi ya wanasasa walio uhamishoni.

Wito huo ulitolewa na rais wakati mamlaka ya mpito ikisonga mbele katika kuandaa mazungumzo ya pamoja yaliyopangwa mwishoni mwa mwaka huu. Wito huo uliitikiwa na baadhi ya watu kutoka makundi hayo, kwani watu 25 walirudi wiki hii nchini Chad, kulingana na Mahamat Doki Warou.

Mshauri huyu wa kisiasa wa rais wa kundi la UFR alirudi mjini Ndjamena Jumanne wiki hii baada ya miaka 20 akiishi nje ya nchi. "Tuliamua kurudi kwa sababu tulifikiri kwa uangalifu juu ya wito wa rais Mahamat Idriss Déby. Kwa sasa, tuna imani na kauli yake. Tuna imani na natumai atakabiliana na changamoto hiyo. Tunarudi baada ya wito wa serikali kuja kusaidia kuijenga nchi yetu. Tunakubali na tuko tayari kwenda kwenye mazungumzo ya kitaifa yasiyobagua. Tunataka kuwaleta pamoja wananchi wote wa Chad ili kuosha nguo chafu kama familia, ”Mahamat Doki Warou ameiambia RFI.

Hata hivyo bado kuna mgawanyiko katika makundi hayo kuhusu wito wa rais Mahamat Idriss Deby. “Tunaamini kwamba hakuna mwanachama wetu aliyeondoka au kujiunga na wito uliotolewa na N'Djamena. Tunajua kwamba mmoja wa makada wetu, Bwana Mahamat Hano, amerejea nchini, lakini mbali na yeye, hakuna kada mwingine kutoka UFR aliyerudi. Hawa ni ndugu wa Chad wanaorudi nchini, ni haki yao kurejea nchini, lakini hilo halituhusu kamwe, "amesema Youssouf Amit, msemaji wa kundi la UFR.

Amebaini kwamba makundi yenye silaha na wanasiasa walio uhamishoni hawajapewa taarifa yoyote rasmi kutoka N'Djamena juu ya ushiriki wao katika mazungumzo ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.