Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Ujumbe wa Libya nchini Chad kujadili usalama wa mipaka

Makamu wa rais wa Baraza la utawala la Libya, Moussa Al-Koné Moussa, na rais wa Baraza la utawala wa kijeshi la Chad, Mahamat Idriss Déby, walifanya mkutano wa faragha Jumatano. Miongoni mwa maswala yaliyojadiliwa: kuzinduliwa tena kwa mipango ya biashara na uchumi kati ya nchi hizo mbili. Lakini pia, masuala ya usalama.

Jenerali Mahamat Idriss Deby, rais wa Baraza la utawala wa kijeshi, katika ikulu ya rais, Aprili 27, 2021 huko Ndjamena.
Jenerali Mahamat Idriss Deby, rais wa Baraza la utawala wa kijeshi, katika ikulu ya rais, Aprili 27, 2021 huko Ndjamena. AFP - BRAHIM ADJI
Matangazo ya kibiashara

Nchini Chad, hii ni ziara ya kwanza ya ujumbe wa Libya tangu kifo cha Rais Idriss Déby. Kupitia mkutano huu, Ndjamena imetangaza azma yake ya kuzindua tena makubaliano ya pande nne kati ya Libya, Sudan, Niger na Chad. Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mnamo mwaka 2018, yanatarajia kuwezesha kuanzishwa kwa vikosi vya pamoja ili kulinda mipaka. Mpaka wa porini wa Chad na Libya unapima zaidi ya kilomita 1,000 ambapo makundi yenye silaha na wanajihadi yanaendesha harakazi zao na kuhatarsha usalama katika nchi hizo mbili.

"Nchi yetu imejitolea kabisa kutekeleza jukumu lake kusaidia raia wa Libya. Lakini Chad inanataka mamluki na vikosi vyenye silaha vivilivyo nchini Libya havitayumbisha usalama katika nchi jirani, ”amesema rais Déby. Ili kuleta utulivu katika eneo hilo, utatuzi wa suala la kutokuepo kwa wanajeshi katika eneo na kupokonya silaha mamluki ni muhimu kwa mamlaka ya Chad.

Kulinda mpaka huu ni suala la kweli kwa Baraza la utawala wa kijesh la Chad. Mwezi Aprili mwaka huu, kundi la waasi la FACT liliondoka Libya kujaribu kupindua mamlaka huko Ndjamena, nchini Chad.

Wataalam kutoka ukanda huo na vile vile mamlaka ya Libya pia mara kwa mara wanaelezea kuhusika kwa mamluki wa Chad katika mzozo wa Libya. Mnamo mwezi wa Julai, wataalam wa Umoja wa Mataifa walitoa wito wa kuondoka kwa mamluki nchini Libya ambao idadi yao inakadiriwa - mataifa yote kwa pamoja - karibu 20,000. Hii "ili kufungua njia kwa amani na uchaguzi" nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.