Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Mahakama kutoa uamuzi kuhusu mauaji ya Thomas Sankara

Mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou inatazamiwa kutoa uamuzi wake Jumatano Aprili 6 katika kesi ya wanaodaiwa kumuua Thomas Sankara. 

Watu wanasubiri kufunguliwa kwa kesi ya wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Thomas Sankara, hatimaye kuahirishwa hadi Oktoba 25, huko Ouagadougou, Oktoba 11, 2021.
Watu wanasubiri kufunguliwa kwa kesi ya wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Thomas Sankara, hatimaye kuahirishwa hadi Oktoba 25, huko Ouagadougou, Oktoba 11, 2021. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Washtakiwa 14 wamefikishwa mahakamani kuhusiana na kesi hii, wakiwemo wawili waliohukumiwa bila kuwepo mahakamani: Rais wa zamani Blaise Compaoré na Hyacinthe Kafando, mkuu wake wa usalama. Wanatuhumiwa kushiriki katika mauaji ya rais wa zamani wa Burkina Faso, baba wa mapinduzi, aliyeuawa na washirika wake 12 mnamo Oktoba 15, 1987. Ndugu wa wahanga wamekuwa wakisubiri uamuzi huu wa mahakama kwa miaka 35.

Ilichukua miaka kadhaa ya uchunguzi, kesi ambayo walihusishwa mashahidi zaidi ya 110 na kesi hii imesikilizwa kwa miezi 6 ya hadi leo. Miaka thelathini na tano baada ya kutokea kwa tukio hilo, ushahidi si wa kutosha. Hakuna picha, hakuna vipimo madhubuti vya DNA, wala sauti, lakini vyeti vichache vya vifo walivyoghushi.

Kwa hiyo upande wa mashtaka uliegemea zaidi ushuhuda, lakini hapa tena, ukungu wa kumbukumbu unabaki kuwa mzito. Ikiwa si kwa Elysée Yamba Ilboudo, dereva wa Blaise Compaoré wakati huo ambaye anakumbuka vizuri kuwabeba kwa gari watu kutoka kundi lililomuua Thomas Sankara kwa jengo kulikokuwa kufanyika kikao cha Baraza la mawaziri Oktoba 15, 1987.

"Tuliondoka nyumbani kwa Blaise Compaoré mwendo wa saa kumi jioni kwa maagizo ya Hyacinthe Kafando," amekumbusha. Kisha watu hao niliobeba walielekea kwenye jengo ambalo Thomas Sankara na washirika wake walikuwa wanakutana. "Nilimwona Sankara akitoka nje huku akiweka juu mikono yake na wakampiga risasi," amesema Elysée Yamba Ilboudo.

Na kisha kuna Abderrahmane Zetyenga, naibu wa zamani wa Jenerali Gilbert Diendéré hatetemeki wakati wa makabiliano yake na mkuu wa zamani wa majeshi wakati wa utawala wa Blaise Compaoré na amekumbusha kila agizo lililotolewa na mkuu wake. Hatimaye Kanali Moussa Diallo, aliyekuwa na cheo cha kanali wakati huo, pia amekumbusha "kiu cha madaraka" cha Blaise Compaoré na Gilbert Diendéré.

Diendéré akanusha shutuma hizo

Jenerali Gilbert Diendéré amefutilia mbali shuhuda nyingi wakati wa aliposikilizwa. Akiwa amesimama, akiwa amevalia sare za jeshi, Gilbert Diendéré alieelezea alichokuwa akikifanya siku hiyo ya Oktoba 17 na kukana tuhuma dhidi yake.

Alipoulizwa kwa nini hakujibu mashambulizi au kuwakamata washambuliaji waliokuwa chini ya amri yake. "Nilikuwa peke yangu, nilinyang'anywa silaha. Ukosefu mdogo na ningekuwa mwathirika wa kumi na nne, "alijitetea mkuu wa zamani wa usalama wa rais. Hata kama toleo lake lilipingwa katika mahakama na Abderrahmane na mashahidi wengine wakati wa makabiliano hayo.

Kwa upande wa Kanali Meja Moussa Diallo, msaidizi wa zamani wa kambi ya Thomas Sankara amesema, "aliyeandaa jambo hili ni Blaise Compaoré, msimamizi wa mapinduzi ni Jenerali Gilbert Diendéré na waliohusika na mauaji ni sehemu ya walinzi wa Blaise Compaoré."

Gilbert Diendéré sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela. Rais wa zamani Blaise Compaoré na Hyacinthe Kafando, wote walio uhamishoni nchini Côte d'Ivoire na ambao hawakuripoti mahakamani, wanakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.