Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mpatanishi wa ECOWAS aondoka Bamako bila makubaliano juu ya tarehe ya uchaguzi

Mpatanishi wa Afrika Magharibi kwa Mali, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, ameondoka Bamako baada ya ziara ya siku mbili bila kupata tarehe ya uchaguzi kutoka kwa serikali ya kijeshi kuhusu raia kurejea tena madarakani, ujumbe wake na chanzo kilicho karibu na serikali ya Mali vimesema.

Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonhatan, na mpatanishi wa Mali, katika mkutano wa ECOWAS mjini Accra, Mei 30, 2021.
Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonhatan, na mpatanishi wa Mali, katika mkutano wa ECOWAS mjini Accra, Mei 30, 2021. AFP - NIPAH DENNIS
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, utawamla wa kijeshi  umetangaza kuwa "uko tayari kwa kipindi cha mpito cha chini ya miaka minne", chanzo kutoka Mali kilicho karibu na mazungumzo na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kimeliambia shirika la habari la AFP, bila hata hivyo kutaja tarehe.

"Tuko mwisho wa ujumbe jijini Bamako. Ikiwa ni kusema kwamba tumekubaliana tarehe ya kumalizika kwa kipindi cha mpito, nitajibu hapana," mmoja wa kati ya wajumbe wanaoongozwa na Bw. Jonathan ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili, ambaye aliwasili Bamako siku ya Ijumaa.

"Ninajua kwamba hakika hakuna, makubaliano ya tarehe" ya uchaguzi yaliyofikiwa, mwishoni mwa mazungumzo haya, chanzo cha kutoka Mali kilicho karibu na mazungumzo hayo, kimeliambia shirika la habari la AFP.

Mpatanishi huyo wa Afrika Magharibi alikuwa ametoa wito wa mabadiliko ya kidemokrasia "haraka iwezekanavyo", siku moja baada ya kupitishwa kwa mpango wa kuruhusu utawala wa kijeshi kusalia madarakani kwa miaka mitano.

Pendekezo la mwisho lililotolewa na utawala wa kijeshi kwa ECOWAS, wakati wa mkutano wa kilele wa mwisho wa jumuiya hiyo ulioshughulikia suala hilo mwanzoni mwa mwezi Februari huko Accra, lilikuwa ni kipindi cha mpito cha miaka minne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.