Pata taarifa kuu
MALI-VIKWAZO

Mali yashindwa kulipa madeni yake baada ya kuchukuliwa vikwazo na ECOWAS

Serikali ya Mali, inayokabiliwa na vikwazo kutoka kwa Jumuaiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, imeshindwa kulipa madeni yake kadhaa katika soko la fedha la Kikanda tangu mwisho wa mwezi wa Januari, kulingana na Umoa-titres, ambayo inasimamia shughuli za masoko ya Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU).

Bamako mji mkuu wa Mali, ambayo imeshindwa kulipa madeni yake baada ya kuchukuliwa vikwazo na ECOWAS.
Bamako mji mkuu wa Mali, ambayo imeshindwa kulipa madeni yake baada ya kuchukuliwa vikwazo na ECOWAS. © Arensond/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Tangu Januari 31, Umoa-titres imechapisha maelezo matano kwa wawekezaji yanayoonyesha kwamba Mali "haijaweza kutatua ahadi zake za kifedha kwenye soko la hisa za umma (MTP)".

Jumla ya kiasi cha kutolipwa kwa kiasi kinachodaiwa ni faranga za CFA bilioni 53, au euro milioni 81.

"Ikumbukwe kwamba tukio hili la malipo linatokea katika hali ambayo nchi ya Mali iko chini ya vikwazo vilivyochukuliwa dhidi yake na mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika magharibi (ECOWAS)" imebaini Umoa-titres katika taarifa yake ya mwisho, siku ya Ijumaa.

Mnamo Februari 2, serikali ya Mali ilitangaza kuwa haijarejesha malipo yanayohusiana na masuala mawili ya bondi kwenye soko la fedha la WAEMU, ambayo ni zaidi ya faranga za CFA bilioni 2.6, "kwa sababu ya vikwazo".

Mali "daima imeheshimu ahadi zake kwenye soko la fedha (na) inataka kuwahakikishia wawekezaji nia yake na uwezo wa kutimiza ahadi zake", iliongeza taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Uchumi na Fedha ya Mali.

Mnamo Januari 9, ECOWAS na UEMOA zilichukua hatua kadhaa kali za kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya Mali ili kuidhinisha nia iliyohusishwa na viongozi wa mapinduzi kusalia madarakani kwa miaka kadhaa zaidi, baada ya majaribuio mawili ya mapinduzi mnamo Agosti 2020 kisha Mei 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.