Pata taarifa kuu

Mali: Mamlaka ya mpito yapitisha mkataba mpya

Mkataba mpya wa mpito nchini Mali umepitishwa kwa kauli moja, Jumatatu, Februari 21 asubuhi, na wajumbe wa Baraza la Kitaifa la Mpito, CNT, ambalo linafanya kazi kama chombo cha kutunga sheria kwa muda nchini humo.

Rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, wakati wa ukaguzi wa vikosi vya jeshi mnamo Juni 7, 2021 huko Bamako.
Rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, wakati wa ukaguzi wa vikosi vya jeshi mnamo Juni 7, 2021 huko Bamako. AFP - ANNIE RISEMBERG
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu, ambao umepitishwa hivi punde na mamlaka, unatoa vipengele vipya kadhaa. Tayari kuna idadi ya wabunge walioteuliwa na ambao hawakuchaguliwa, na hivyo idadi hiyo inatoka kwa wabunge 121 hadi 147, na kwa kipindi cha mpito tu. Katika nakala hiyo, pia imeandikwa kuwa uchaguzi ujao wa urais, ambao tarehe yake bado haijajulikana, ndiyo utakayoashiria mwisho wa kipindi cha mpito.

Nafasi ya makamu wa rais wa mpito imefutwa. Kabla ya mapinduzi ya pili ya Mei 2021, Assimi Goïta, mkuu wa sasa wa nchi, ndiye alichukua madaraka. Katika katiba mpya, imeelezwa kuwa kama rais wa mpito, Kanali Goïta hataweza kuwania uchaguzi ujao wa rais na wa wabunge. Hatimaye, kuna msamaha uliopigiwa kura kwa wahusika wa mapinduzi mawili ya mwisho.

Kuhusu kipindi cha mpito, mkataba mpya hautaji tarehe mahususi ya mwisho. Ni kwamba maoni yanatofautiana juu ya suala hili. Muswada uliowasilishwa na kipindi cha mpito unajumuisha kipindi cha kati ya miezi sita na miaka mitano, kama ilivyopendekezwa na majadiliano ya kitaifa.

Hatimaye, mijadala bado inaendelea. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), linazingatia miezi kumi na mbili kama tarehe ya mwisho, mwenyekiti wa taasisi hiyo ya kikanda alisema hivi majuzi. Lakini katika maelezo mengine ya kiufundi, waraka wa kazi kutoka kwa washirika kadhaa wa Mali (ECOWAS, UN, Umoja wa Afrika), kuna mipango miwili kama msingi wa mazungumzo: kipindi cha mpito cha miezi kumi na mbili, na mpango wa pili: kipindi cha mpito cha miezi kumi na sita kabla ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.