Pata taarifa kuu

Ufaransa na washirika wake "kuondoka" nchini Mali

Baada ya chakula cha jioni katika Ikulu ya Élysée kilichohudhuriwa na baadhi ya viongozi thelathini wa Afrika na Ulaya, Ufaransa, washirika wake wa Ulaya na Canada walitangaza, Alhamisi, Februari 17, kuondolewa kwa vikosi vya kijeshi nchini Mali baada ya kusaidia vikosi vya nchi hio kwa miaka tisa.

Katika picha hii ya zamani ya Jumatano, Juni 9, 2021, wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane, ambao wamemaliza huduma yao ya miezi minne katika ukanda Sahel, wanaondoka kambi yao huko Gao, Mali.
Katika picha hii ya zamani ya Jumatano, Juni 9, 2021, wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane, ambao wamemaliza huduma yao ya miezi minne katika ukanda Sahel, wanaondoka kambi yao huko Gao, Mali. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa baada ya mkutano wa Jumatano jioni huko Élysée kati ya washirika wa Afrika na Ulaya kujadili hali ya ukanda wa Sahel ambapo uamuzi huo uliidhinishwa. Vikosi vya Barkhane na Takuba kwa hivyo vitaondoka Mali "kwa wakati mmoja".

"Kutokana na vikwazo vingi vya mamlaka ya mpito ya Mali", nchi hizo zinaamini kuwa masharti ya kisiasa, kiutendaji na kisheria hayatimizwi tena ili kutekeleza dhamira yao ya kijeshi ya sasa. "Tunaendelea kuunga mkono Mali na raia wake katika juhudi zao za kufikia amani na utulivu wa kudumu", inabainisha nakala ya tamko hili la pamoja.

"Kujiondoa huku kutasababisha kufungwa kwa barabara za Gossi, Ménaka na Gao, na zoezi hili ltafanywa kwa utaratibu mzuri, pamoja na wanajeshi wa Mali na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali", mkuu wa majeshi ya Ufaransa amebainisha.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu kuondoka huku kwa wanajeshi, rais wa Ufaransa amebaini kwamba "anakataa kabisa" dhana ya kushindwa nchini Mali.

Kuongeza msaada wa kijeshi kwa nchi jirani za Afrika Magharibi

Nchi zilizotia saini zimekubali kuendelea na hatua yao dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel, hasa katika nchi ya Niger na Ghuba ya Guinea, maeneo ambayo yamekuwa "vipaumbele vya mkakati wa upanuzi" wa al-Qaeda na kundi la Islamic State," Rais Emmanuel Macron amesema.

Mashauriano ya kisiasa na kijeshi yameanzishwa na nchi husika ili kuweka, ifikapo Juni 2022, "vigezo vya hatua hii ya pamoja" , ameongeza rais wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.