Pata taarifa kuu

Le Drian: Ufaransa itaendelea kupambana na ugaidi katika Sahel, lakini sio nchini Mali

Kauli hizi, jana jioni kwenye Ufaransa 5, zimekuja saa chache baada ya mkutano wa video wa mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya na katika mkesha wa mkutano kati ya Emmanuel Macron na wenzake watatu kutoka ukanda wa Sahel: Niger Mohamed Bazoum, Mahamat Idriss Déby wa Chad na Mohamed ould Ghazouani wa Mauritania.

Kikosi kazi cha Takuba kimetumwa nchini Mali.
Kikosi kazi cha Takuba kimetumwa nchini Mali. © AFP/Thomas Coex
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Ufaransa alitaka tujipange upya lakini hatuondoki," amebaini Jean-Yves Le Drian. "Ikiwa masharti hayatatimizwa tena ili tuweze kuchukua hatua nchini Mali, tutaendelea kupambana na ugaidi pamoja, na nchi zingine za Sahel ambazo zinataka ushirikiao huo", ambainisha waziri wa Mambo ya Nje ya Ufaransa.

Kulingana na Paris, masharti hayajatimizwa kwa Ufaransa kuendelea na harakati zake za kijeshi nchini Mali. Htau ay viongozi wa mapinduzi kuendelea kusalia madarakani na kuwasili kwa mamluki wa kampuni ya Urusi ya Wagner, ambao Jean-Yves Le Drian anakadiria kuwa wanafikia idadi ya 1,000 leo, inaonekana Mali imevuka mistari nyekundu, ambayo Ufaransa haiwezi kuvumilia.

Mgogoro na Mali unaweka hatua ngumu kwa Ufaransa kuendelea na harakati zake za kijeshi nchini Mali. Baada ya kazi ndefu ya kidiplomasia ya Ufaransa, nchi kadhaa za Ulaya sasa zimechangia kutuma wanajeshi katika kikosi kazi cha Takuba, kundi la vikosi maalum ambavyo vilipaswa kuchukua nafasi ya Barkhane. Tangazo la kujiondoa kutoka Mali kwa hivyo litakomesha uzoefu wa kipekee, ambao Paris ilijivunia.

Chanzo kilicho karibu na Ikulu ya Élysée kinathibitisha kuwa nchi washirika zingependa kuendeleza harakati hii lakini wapi? Niger, ambayo tngu mwezi wa Novemba 2020 imepokea uongozi wa Barkhane na washirika wake kutoka ukanda wa Shael, haijavutiwa sana na wazo hilo. Mauritania hadi sasa haijaonesha msimamo wake dhidi ya hali ya Mali.

Kuhusu Burkina Faso, sintofahamu bado ni kubwa tangu mapinduzi ya Januari 24. Ingawa makao makuu ya jeshi la Ufaransa huzidisha miito k

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.