Pata taarifa kuu

Wiki muhimu kwa ahadi ya Ufaransa na Ulaya kwa Sahel

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya umepangwa kufanyika Jumatatu tarehe 14 Februari. Unatangulia mikutano mingine mikuu ya kidiplomasia iliyopangwa kufanyika wiki hii. Matangazo yanatarajiwa juu ya uwezekano wa kujiondoa kwa wanajeshi wa Ufaransa na wale wa Ulaya waliotumwa kusaidia nchini Mali na juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijeshi.

Kikosi cha Takuba (picha), kilichoundwa kusaidia Mali katika mapambano yake dhidi ya wanajihadi kinajumuisha wanajeshi kutoka nchi kumi na tano za Ulaya.
Kikosi cha Takuba (picha), kilichoundwa kusaidia Mali katika mapambano yake dhidi ya wanajihadi kinajumuisha wanajeshi kutoka nchi kumi na tano za Ulaya. Thomas COEX AFP
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya wanakutana kwa njia ya video Jumatatu tarehe 14 Februari. Mashauriano makali yaliyoanzishwa kwa zaidi ya wiki mbili juu ya mustakabali wa kikosi cha Takuba, kinachoundwa na takriban nchi kumi na tano za Ulaya ambazo zilijitolea kuchangia kwa kwa kikosi hiki, na ujumbe wa mafunzo ya kijeshi wa Umoja wa Ulaya EUTM, yataendelea. "Kuna wale ambao wanataka kudumisha uwepo wao nchini Mali ili wasiache nafasi kwa Urusi", kimeleza chanzo cha kidiplomasia, na wale ambao wanataka kuondoka kabisa.

Matangazo kutolewa siku ya Jumatano

Lakini siku inayojulikana ni Jumatano: Emmanuel Macron amewaalika wakuu wa nchi za G5 Sahel mjini Paris: Rais wa Niger Mohamed Bazoum, Mahamat Idriss Déby wa Chad na Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania. Mamlaka ya mpito za kijeshi za Burkina Faso na Mali, zilizotokana na mapinduzi ya kijeshi ya Januari 24, hazikualikwa.

Mwenyekitiwa Umoja wa Afrika, Macky Sall ambaye ni rais wa Senegal, Mwenyekiti wa ECOWAS, ambaye ni fais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Rias wa Baraza la Ulaya Charles Michel, na mkuu wa sera za Mamabo ya Nje ya Ulaya Josep Borrell pia wanatarajiwa kuhudhuria kikao hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.