Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali: Mpatanishi wa ECOWAS kuzuru Bamako

Ujumbe kutoka ECOWAS unatarajiwa Ijumaa hii, Machi 18, 2022, mjini Bamako. Mpatanishi wa Mali kwa niaba ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, Goodluck Jonathan, atajaribu kwa mara nyingine kukubaliana na mamlaka ya mpito kuhusu ratiba ya uchaguzi kwa lengo la kurejeshwa kwa kikatiba ya nchi ya Mali. Uchaguzi wa urais na wa wabunge, uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Februari, haukufanyika.

Rais wa zamani Goodluck Jonathan, mpatanishi wa ECOWAS wakati wa ziara yake huko huko Bamako, Mali, Mei 25, 2021.
Rais wa zamani Goodluck Jonathan, mpatanishi wa ECOWAS wakati wa ziara yake huko huko Bamako, Mali, Mei 25, 2021. REUTERS - AMADOU KEITA
Matangazo ya kibiashara

Mali imekuwa ikiishi chini ya vikwazo vya kiuchumi na kifedha kwa muda wa miezi miwili na nusu, na mamlaka inatafuta kuondolewa kwa vikwazo hivi ambavyo vinawaadhibu pakubwa raia wake.

Siku ya Alhamisi, Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, rais wa Senegal Macky Sall, alisema alikutana na rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, "siku moja kabla" ya ziara ya mpatanishi. "Naunga mkono kuanzishwa tena kwa mazungumzo kwa ajili ya suluhu la mzozo nchini Mali," alisema Rais Macky Sall. Umoja wa Afrika tayari umeeleza msimamo wake: kuongezwa kwa kipindi cha mpito kwa muda usiozidi miezi kumi na sita. ECOWAS inataka kuongezewa muda mfupi, miezi kumi na miwili. Huu ni muda unaochukuliwa kuwa "unakubalika" na Nana Akufo-Addo wa Ghana, Mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS.

Kwa upande wa mamlaka ya Bamako, baada ya pendekezo la awali la miaka mitano, lililopunguzwa hadi miaka minne mwanzoni mwa mwezi wa Januari, matamko mengi yametolewa yanayoashiria uwazi wa maelewano, ili kupata kuondolewa kwa vikwazo vya ECOWAS haraka iwezekanavyo. Baadhi ya vyanzo vinabaini kwamba kuongezw kwa miezi ishirini na nne inaweza kupendekezwa na mamlaka ya mpito ya Mali kwa mpatanishi wa ECOWAS, ambayo haijathibitishwa rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.