Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Adriano Afonso Maleiane ateuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Msumbiji

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amemteua Adriano Afonso Maleiane kuwa Waziri Mkuu mpya, baada ya kulifanyia mabadiliko Baraza lake la Mawaziri wiki hii. 

Filipe Nyusi, rais wa Msumbiji.
Filipe Nyusi, rais wa Msumbiji. Tiziana FABI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maleiane anachukua nafasi ya Carlos Agostinho do Rosário,ambaye amekuwa katika nafasi hiyo tangu mwaka 2015 hadi alipoondolewa katika nafasi hiyo. 

Uteuzi mwingine uliofanyika ni wa Ernesto Max Tonela ambaye ndio Waziri mpya wa Uchumi na fedha pamoja na Carlos Zacarias, ambaye sasa atakuwa Waziri wa nishati. 

Siku ya Jumatano, Nyusi aliwafuta kazi Waziri wake sita, bila ya kutoa sabababu, hatua ambayo imeelezwa kuwa mabadiliko makubwa ya serikali yake. 

Wachambuzi wa siasa za Msumbiji wanasema, hatua hii huenda imechochewa pakubwa na kesi ya ufisadi kuhusu wizi wa Dola Bilioni 2 inayowahusiska maafisa 19 wa juu wa serikali nchini humo. 

Mabadiliko haya yanatoa nafasi kwa Nyusi kuwateuwa washirika wapya watakaomtetea kuelekea mkutano wa chama tawala cha Frelimo mwezi Septemba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.