Pata taarifa kuu

Mfalme wa Ubelgiji Philippe kuzuru DRC mwanzoni mwa mwezi wa Machi

Mfalme wa Ubelgiji Philippe, ambaye mnamo 2020 alielezea "masikitiko" yake kuhusu usimamizi wa nchi yake katika enzi za ukoloni, atafanya ziara yake ya kwanza rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia Machi 6 hadi 10, Ikulu imeitangaza Jumatano Februari 16.

Rais wa drc Félix Tshisekedi akiwa na Philippe, Mfalme wa Ubelgiji, kwenye Kasri  la Kifalme huko Brussels, Septemba 17, 2019.
Rais wa drc Félix Tshisekedi akiwa na Philippe, Mfalme wa Ubelgiji, kwenye Kasri la Kifalme huko Brussels, Septemba 17, 2019. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Philippe ataandamana na mkewe, Malkia Mathilde, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo, Waziri wa Mambo ya Nje Sophie Wilmès na Waziri wa Ushirikiano kwa Maendeleo Meryame Kitir, Ikulu imesema katika taarifa.

Pia itakuwa ni ziara ya kwanza ya kifalme ya Ubelgiji nchini DRC tangu ziara ya Albert II, babake Philippe, mwaka 2010, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa koloni hilo la zamani la Ubelgiji.

Mnamo mwezi Juni 2020, Mfalme Philippe, ambaye ametawala tangu 2013, alielezea kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi "maqsikitiko yake makubwa kwa majeraha" waliyoyapata raia wa DRC wakati wa ukoloni wa Ubelgiji nchini Kongo (DRC ya sasa).

Maelewano muhimu

Katika barua aliyoituma kwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, alielezea "masikitiko yake makubwa kwa majeraha haya ya siku zilizopita, ambayo maumivu yake leo yanachochewa na ubaguzi ambao bado uko katika jamii zetu".

Aidha, Ubelgiji inajiandaa kurudisha mjini Kinshasa jino la Patrice Lumumba, shujaa wa Kongo wa mapambano dhidi ya ukoloni na Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo huru, ambaye mwili wake, uliyeyushwa kwa tindikali, haujawahi kupatikana. Sherehe ya kurudisha "mabaki" haya, iliyokuwa imepangwa kufanyika mwezi wa Juni 2021 huko Brussels, iliahirishwa kwa sababu ya janga la COVID-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.