Pata taarifa kuu
UBELGIJI-USHIRIKIANO

Mpango wa kurejesha mabaki ya Patrice Lumumba waahirishwa

Mamlaka ya Ubelgiji imeahirisha mpango wa  kurejesha mabaki ya muasisi wa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza, Patrice Lumumba kwa familia yake kama ilivyokuwa imepangwa kuwa tukio hilo lingefanyika siku ya Jumamosi Januari 8 mwaka huu.

Patrice Lumumba (Katikati) wakati wa harakati za uhuru mwaka 1960
Patrice Lumumba (Katikati) wakati wa harakati za uhuru mwaka 1960 AFP PHOTO / STRINGER STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kidiplomasia vimesema hatua ya kuahirisha tukio hilo ambapo ni jino pekee ndilo  lililoonekana baada ya mwili wake kuchomwa katika tindikali, zimeahirishwa kufwatia ombi la serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Tukio hilo la kihistoria, lilikuwa lifanyike Juni 21, mwaka uliopita na liliahirishwa mpaka Januari 2022, miaka 61 ya kifo cha Lumumba.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander de Croo, amekuwa akisema  kuwa nchi yake imeweka wazi kilichotokea hadi kuuawa kwa Lumumba.

Sababu iliyotolewa wakati huo ilikuwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya Janga la Covid-19 ambayo pia wakuu wa DRC wamesema pia ni kwa mwaka Huu.

Binti wake waziri mkuu huyo wa zamani Juliana Lumumba, pia amethibitisha kuwa hivi karibuni alipewa taarifa ya kuahirishwa kwa sherehe hizo na ubalozi wa Ubelgiji nchini DRC, hatua ambayo hata hivyo anasema inashangaza kwa kiasi fulani kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya moja kwa moja na mamlaka ya DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.