Pata taarifa kuu

Gambia: Wanajeshi saba wa Senegal waliokuwa mateka wa MFDC huko Casamance waachiliwa

Nchini Gambia, wanajeshi saba kutoka ujumbe wa Afrika Magharibi nchini Gambia waliachiliwa huru Jumatatu, Februari 14 mchana, na waasi wa Casamance. Walikuwa wamezuiliwa mateka tangu makabiliano yaliyotokea Januari 24.

Wanajeshi wa Senegal kutoka kikos cha ECOWAS walitumwa Gambia.
Wanajeshi wa Senegal kutoka kikos cha ECOWAS walitumwa Gambia. AFP - CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wote saba walionekana wenye afya nzuri, salama salimini. Waliwasili bila kuwa na silaha zao, wakiwa wamezungukwa na waasi. Makabidhiano ya wafungwa wa Ecomig yalifanyika katika maeneo ya mashambani, karibu na mpaka na Senegal, anasema mwandishi wetu wa habari huko Banjul, Milan Breckmans.

Kiongozi wa waasi Salif Sadio hakuhudhuri sherehe hiyo, lakini pia mamlaka ya Dakar na Banjul ambao hawakutuma wawakilishi. Baadhi ya watu walifunga safari, kupitia njia hatarishi katikati ya msitu. Kando ya mwakilishi wa ECOWAS walikuwepo wajumbe wawili wa ICRC, pamoja na kiongozi wa jumuiya ya Sant'Egidio, jumuiya ambayo ilifanya kazi kama mpatanishi ili kuweza kuachiliwa kwa mateka hao.

Hotuba hizo zilitanguliwa na kauli za kupongeza: bila kutoa neno lolote, kila askari alitia saini kwenye karatasi inayothibitisha kuachiliwa kwake. Hati iliyotiwa saini tena na Mnigeria Claude Kondor, aliyewakilisha ECOWAS. Alishukuru kwa moyo mkunjufu MFDC kwa hatua hioyo: "Tumeona vita katika baadhi ya nchi, lakini ishara kama hizo hazijawahi kuonekana. Kwa niaba ya ECOWAS, ninataka kukushukuru kwa ishara hii ambayo ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu. »

Wanajeshi hao saba walikuwa wameshikiliwa mateka tangu makabiliano ya Januari 24 kati ya kikosi cha ECOWAS na waasi wa MFDC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.