Pata taarifa kuu

Gambia: Wanajeshi wawili wa Senegal wa kikosi cha ECOWAS wauawa katika shambulio

Nchini Senegal, jeshi limetangaza kifo cha wanajeshi wawili waliotumwa katika nchi jirani ya Gambia, katika kikosi cha Ecomig, kikosi cha ECOWAS.

Wanajeshi wa Ecomig nchini Gambia. Ujumbe huu ulianzishwa baada ya mkwamo wa kisiasa wa mwaka 2017 na kukataa kwa Yahya Jammeh kuachia madaraka.
Wanajeshi wa Ecomig nchini Gambia. Ujumbe huu ulianzishwa baada ya mkwamo wa kisiasa wa mwaka 2017 na kukataa kwa Yahya Jammeh kuachia madaraka. CARL DE SOUZA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na makao makuu ya jeshi huko Dakar, wanajeshi hao waliokuwa wakifanya doria washambuliwa Jumatatu, Januari 24, 2021, na watu wenye silaha "wanaodhaniwa kuwa" wa kundi la waasi la Casamance, MFDC.

"Shambulio la ukubwa huu dhidi ya kikosi cha Ecomig halijawahi kutokea," amesema mmoja wa watu wanaotambua vema eneo hilo, ambaye alisema kuwa eneo la Bwiam, kusini mwa Gambia, liko karibu na ngome ya kundi la MFDC linaloongozwa na Salif Sadio. Amekumbusha kwamba wapiganaji kundi hilo "hapo awali walishutumu jeshi la Senegal lililowekwa katika ujumbe wa ECOWAS kwa kufanya uvamizi kutoka nchini Gambia".

Majeshi ya Ecomig yaliwekwa katika eneo la Bwiam kusini mwa Gambia, imebaini idara ya habari na uhusiano wa umma wa majeshi (Dirpa) huko Dakar, baada ya shambulio lililogharimu maisha ya wanajeshi wawili wa Senegal Jumatatu hii, Januari 24.

Mwaka mmoja uliopita, jeshi la Senegal lilianzisha operesheni kubwa kusini mwa Casamance - kwenye mpaka na Guinea-Bissau - dhidi ya ngome za kihistoria za MFDC, kundi la waasi lililogawanyika sana. Mazungumzo na serikali, yaliyozinduliwa tena mnamo 2012, hayakuzaa makubaliano ya uhakika ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.