Pata taarifa kuu
SENEGAL-USALAMA

Utafiti Senegal: Ripoti ya ISS yaelezea dosari za kiusalama kwenye mpaka wa Mali

Katika mazingira ya kikanda yenye machafuko, Senegal hadi sasa imeepushwa na mashambulizi ya kigaidi. Lakini ripoti mpya inaonyesha "udhaifu" katika mikoa ya Tambacounda na Kédougou, kwenye mpaka na Mali.

Wanajeshi wa Senegal wakishika doria.
Wanajeshi wa Senegal wakishika doria. © Charlotte Idrac
Matangazo ya kibiashara

Senegal ni nchi "inayokabiliwa na shinikizo la usalama," kulingana na utafiti huu uliochapishwa Alhamisi, Desemba 16, na Taasisi ya Mafunzo ya Usalama (ISS) na Kituo cha Mafunzo ya Juu ya Ulinzi na Usalama (CHEDS). Hali inayohusishwa na uchimbaji wa dhahabu katika eneo hilo.

Hali ngumu, ukosefu wa miundombinu, usafirishaji haramu wa binadamu, matukio ya hapa na pale kati ya jamii zinazoendesha shughuli za uchimbaji dhahabu katika eneo la Kedougou ... Haya yote ni mambo ambayo makundi yenye itikadi kali kutoka Mali yanaweza kunufaika nayo, kulingana na waandishi wa ripoti hiyo.

“Kutokana na ukweli kwamba taifa la Senegal halina udhibiti kamili wa uzalishaji wa dhahabu katika eneo hilo, lakini pia katika mzunguko wa soko, inaonekana kuwa hii ni mianya ambayo makundi haya yanaweza kutumia ili kupata rasilimali za kifedha, lakini pia kutumia sekta hii ili kupata rasilimali za kiuendeshaji, kama wanavyofanya katika baadhi ya nchi katika ukanda wa Sahel ”, anaelezea Paulin Maurice Toupane, mtafiti mkuu katika kituo cha ISS.

Senegal imeimarisha mfumo wa usalama kusini-mashariki mwa nchi. Lakini jibu lazima liwe na sura nyingi, inasisitiza ripoti hiyo: "Nchi ya Senegal inapaswa kutekeleza idadi ya mipango ili sio tu kupunguza udhaifu wa kijamii na kiuchumi ambao huchochea hisia za kuchanganyikiwa na kutengwa ambazo zina nguvu sana katika baadhi ya maeneo la maeneo. Senegal inapaswa kuchukua hatua kadhaa ili kupunguza mienendo ya migogoro katika eneo hilo, ambayo inahusu upatikanaji wa rasilimali ya madini"

"Inabidi kuchukuwa hatua haraka", amehitimisha mtafiti huyu, "ili kuepuka hali mbaya zaidi katika eneo hilo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.