Pata taarifa kuu

Senegal yaitaka China kusaidi katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi Sahel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Aissata Tall Sall ameitaka China kujitokeza ili kusaidia katika mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel.

Rais Xi Jinping wa China akiwa na mwenzake wa Senegal Macky Sall katika ziara ya kiserikali mjini Dakar mwaka 2018.
Rais Xi Jinping wa China akiwa na mwenzake wa Senegal Macky Sall katika ziara ya kiserikali mjini Dakar mwaka 2018. © AP Photo/Xaume Olleros
Matangazo ya kibiashara

Wito huu umetolewa katika mkutano kati ya China na viongozi wa bara la Afrika jijini Dakar, unaozungumzia masuala mbalimbali, likiwemo suala la ushirikiano wa kiuchumi.

Mkutano huu unfanyika wakati huu, China ikiendelea kutoa mkopo kwa mataifa ya Afrika kwa ajili ya maendeleo.

Kwa hivyo Beijing haipuuzi athari za matangazo na mawasiliano. China inawekeza zaidi kwenye viwanda, madini, ujenzi na usafirishaji. Mwishoni mwa mwaka 2020, kulingana na mamlaka ya China, dola bilioni 43 ziliingizwa bara Afrika kupitia kampuni za China. Kampuni 3,500 inasemekana zilianzishwa barani Afrika.

Kuhusu suala la deni, takwimu zinatofautiana na ni vigumu kujua kiwango kamili cha madeni ya mataifa ya Afrika. Kati ya mwaka 2000 na 2019, China ilikopesha nchi za bara hilo euro bilioni 153 kulingana na taasisi ya China ya China Africa Research Initiative. Lakini dai hili linatofautiana sana kutoka nchi moja hadi nyingine. Angola pekee ina 30% ya deni hilo. Tangu 2016, kiasi cha mikopo kimekuwa kikipungua. Na katika miezi ya hivi karibuni, China imekubali kufuta au kutathmini tena deni la baadhi ya nchi za Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.