Pata taarifa kuu

Senegal: Mkuu wa MFDC aishutumu ECOWAS kuwa chanzo cha mvutano

Wakati wa mapigano yaliyotokea Januari 24 na waasi wa MFDC, wanajeshi wanne wa Senegal waliuawa, kulingana na makao makuu ya jeshi huko Dakar, na wengine saba bado wanashikiliwa mateka na kundi la waasi huko Casamance, karibu na mpaka wa Gambia.

Misitu ya Casamance, Senegal ni maeneo yenye utajiri, lakini pia ni hifadhi ya waasi wa MFDC.
Misitu ya Casamance, Senegal ni maeneo yenye utajiri, lakini pia ni hifadhi ya waasi wa MFDC. Mathieu Damman/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Katika eneo la makabiliano, RFI imeweza kukutana na kiongozi wa waasi Salif Sadio, ambaye anawashutumu wanajeshi wa kikosi cha ECOWAS kuwa sababu ya makabiliano hayo.Baada ya mwendo wa saa kadhaa msituni, hatimaye waandishi wa RFI waliwasilia Bajagar, mji wa Casamance ulio karibu na mpaka wa Gambia. Ni katika eneo hilo ambapo Salif Sadio, kiongozi wa waasi wa MFDC na wapiganaji wake wameweka moja ya kambi zao.

Akihojiwa na RFI, kiongozi wa waasi amerejelea mapigano ya Januari 24.

“Kitu cha kusikitisha kilitokea. Wanajeshi wenye silaha kutoka eneo la Gambia walikuja kushambulia kambi zetu, wakiwa na silaha nzito. Wakati wa shambulio hili, tuliua wanajeshi wawili na tunawashikilia wengine saba, ambao tuliwakamata wakiwa na silaha mkononi. Wanajeshi hao, kila mmoja alisema ni sehemu ya wanajeshi wa ECOWAS, walioko nchini Gambia. Kwa malengo gani: kulinda serikali iliyopo madarakani, ndivyo walivyosema ... Hata hivyo, nina wafungwa saba hapa mnaponiona; mapigano yalitokea katika eneo la Casamance, walivuka mpaka kuja kunishambulia; Nilirudisha miili ya askari waliouawa kwa ECOWAS kwa sababu ECOWAS ilipotambua kuwa walikuwa wanajeshi wake, ilibidi tuwarudishie miili ya askari wao…”

Nini kitatokea sasa? Je, Salif Sadio yuko tayari kuwaachia wafungwa hawa na kwa masharti gani? "Sijui nitawarejesha kwa nani ikiwa sio ECOWAS," amejibu kiongozi wa waasi. (Hao ndio) wahusika hata hivyo! Kwa sababu ikiwa wajumbe wao watapendezwa kuja kuzungumza nami. Ikiwa masharti yatakamilika, wataachiliwa huru mara moja. Mnamo 2012, nilirudisha wafungwa wa Senegal - kutoka jeshi la Senegal - bila masharti! Kama kweli Senegal wamejitolea kujadili, kukaa chini kuzungumza kwa amani, kuzungumza kwa amani na MFDC kutatua tatizo la Casamance, tatizo liko wapi, wafungwa nitawarudisha kwao! »

Salif Sadio alikuwa ameanzisha mazungumzo ya amani. Kulingana na mkuu wa MFDC, mapigano ya Januari 24 yanaweza kuhatarisha makubaliano, lakini hayawezi kusimamisha mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.