Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Burkina Faso: Kesi ya mauaji ya Thomas Sankara yaanza bila mshukiwa mkuu kuwepo

Kesi dhidi ya watu 14 akiwemo rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore, wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya Thomas Sankara kiongozi wa zamani wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, miaka 34 iliyopita, imeanza kusikilizwa kwenye Mahakama ya kijeshi jijini Ouagadougou.

Watu wakihudhuria ufunguzi wa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya Thomas Sankara huko Ouagadougou Oktoba 11, 2021.
Watu wakihudhuria ufunguzi wa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya Thomas Sankara huko Ouagadougou Oktoba 11, 2021. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Washuliwa 12 kati ya 14 walikuwepo Mahakamani siku ya Jumatatu akiwemo, Jenerali Gilbert Diendere, aliyekuwa afisa wa jeshi wakati wa maujai hayo.

Wakili wa washtakiwa hao Mamadou Coulibaly, anasema baadhi ya wateja wake wamechoka na anaomba iwapo kesi hiyo ingeedeshwa kwa mfumo wa video.

Hata hivyo, mshukiwa mkuu rais wa zamani Compaore aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 27 kabla ya kuondolewa madarakani kufuatia maandamano ya wananchi na kukimbilia nchini Côte d’Ivoire, hatofika mahakamani kusikiliza mashtaka dhidi yake, kwa mujibu wa mawakili wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.