ETHIOPIA
Waasi wa Tigray wailalamikia AU kwa kuegemea upande wa serikali
Waasi wa jimbo la Tigray nchini Ethiopia, wanaushtumu Umoja wa Afrika kwa kuegemea upande mmoja kuhusu mzozo unapendelea kufuatia uteuzi wa rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kuwa msuluhishi.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Msemaji wa TPLF, Getachew Reda ameushutumu Umoja wa Afrika kwa kugemea upande wa serikali ya Ethiopia na kuongeza kuwa, hakuna matumaini ya mwafaka kupatikana.
Awali, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alikuwa amekataa wito wa Umoja wa Afrika kusaidia katiika mzozo huo na kutuma wanajeshi katika jimbo hilo mwezi Novemba mwaka uliopita.