Pata taarifa kuu
ZAMBIA

SADC yapongeza uchaguzi wa Zambia

Jumuiya ya Kiuchumi ya mataifa ya Kusini mwa bara Afrika Afrika SADC, imesifia hatua ya viongozi wa Zambia kuhakikisha kuwa kuna makabidhiano ya amani ya madaraka, baada ya kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema kumshinda rais Edgar Lungu katika Uchaguzi wa urais.

Hakainde Hichilema, rais mteule wa Zambia.
Hakainde Hichilema, rais mteule wa Zambia. © REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti mpya wa SADC, Jumuiya ya mataifa 16 , rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, amesema kinachoshuhudiwa nchini Zambia ni mfano wa kuigwa na kupongezwa.

Hatua hii ya kukabidhiana madaraka kwa alani, imekuwa ikishuhudiwa kwenye ukanda wetu katika miaka ya hivi karibuni, Zambia imekuwa nchi nya hivi punde kufuata mfano huu, na hili  ni suala la kuigwa na kupongezwa duniani; kwa viongozi wote wa Zambia, tunasema, Asante.

Siku moja baada ya ushindi wa upinzani nchini Zambia, chama tawala cha zamani, Patriotic Front, kinakabiliwa na mgawanyiko. Wanachama kadhaa wamekihama chama hicho na kujiunga na chama  kilichoshinda uchaguzi cha UPND cha Hakainde Hichilema.

Charles Kakoma, kiongozi mwenye ushawishi katika chama cha Patriotic Front cha Edgar Chagwa Lungu, tayari ametangaza kujiunga na chama cha UPND.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.