Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Zambia: Hakainde Hichalema ashinda uchaguzi kwa kura nyingi

Mwanasiasa mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, 59, ameibuka mshindi wa uchaguzi uliofanyika Agosti 12 dhidi ya rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu, tume ya uchaguzi imetangaza mapema Jumatatu (Agosti 16).

Mgombea wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ameshinda uchaguzi wa urais.
Mgombea wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ameshinda uchaguzi wa urais. SALIM DAWOOD AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ninamtangaza Hakainde Hichilema rais mteule wa Jamhuri ya Zambia Agosti 16," Esau Chulu, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, ametangaza karibu saa 8:30 usiku mbele ya waandishi wa habari.

Amemshinda mpinzani wake, rais aliye madarakani Edgar Lungu, kwa kupata kura milioni 2.8, sawa na kura milioni moja ikilinganishwa na alizopata rais aliye madarakani.

Ni eneo moja tu kati ya maeneo 156 katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambayo kura zake hazijahesabiwa rasmi, lakini tume hiyo imebaini kwamba hata kama kura hizo hazijahesabiwa, hilo haliwezi "kuvuruga ushindi wa Hichilema.

Ushindi uliosherehekewa sana

Hii ilikuwa mara ya tatu Bwana Hichilema kumenyana katika uchaguzi wa urais na Bwana Lungu. Mnamo 2016, alipoteza kura 100,000 tu.

Katika mji mkuu Lusaka, mamia ya wafuasi walikuwa tayari wamekusanyika mapema jioni, ikiwa ni pamoja na mbele ya nyumba ya Bwana Hichilema. Walivaa nguo nyekundu, rangi ya chama chake cha UPND, walicheza, wakapiga honi, walisherehekea ushindi hata kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwana tume huru ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.