Pata taarifa kuu
ZAMBIA-MATOKEO

Mgombea mkuu wa upinzani Hakainde Hichilema aongoza nchini Zambia

Mgombea mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema amechukua uongozi wa mapema kwenye Uchaguzi wa urais dhidi ya rais Edgar Lungu baada ya Tume ya Uchaguzi kuanza kutangaza matokeo siku ya Jumamosi.

Kura zinahesabiwa kwenye uchaguzi wenye ushindani mkali nchini Zambia
Kura zinahesabiwa kwenye uchaguzi wenye ushindani mkali nchini Zambia MARCO LONGARI AFP
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya Tume ya Uchaguzi kutoka maeneo Bunge 15 kati ya 156 yaliyotangazwa Jumamosi asubuhi, yanaonesha kuwa Hichilema anaongoza kwa kura 171,604 dhidi ya rais Lungu ambaye amepata kura 110,178.

Maeneo bunge 15 aliyopata ushindi Hichilema, ni pamoja na ngome za rais Lungu, ambazo alishinda wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2016.

Katika maeneo bunge yenye ushindani mkali kama Chawama jijini Lusaka, chama cha rais Lungu na kile cha Hichilema vyote vimedai kushinda.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kufahamika katika siku chache zijazo huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya rais Lungu na Hichilema.

Katika hatua nyingine, Internet imerejeshwa tena nchini humo na watu wameanza tena kutumia mitandao ya kijamii kama WhatsApp ambayo iliyokuwa imezuiwa siku ya Alhamisi na Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.