Pata taarifa kuu
ESWATINI - USALAMA - SIASA

Wanajeshi wakabiliana na wandamanaji Eswatini

Mamlaka nchini Eswatini, usiku wa kuamkia leo, zimewatumia wanajeshi kuwakabili wandamanaji wanaondamana dhidi ya serikali wakishinikiza mabadiliko ya katiba na demokrasia.

Mfalme wa Eswatini Mswati III na mkewe
Mfalme wa Eswatini Mswati III na mkewe Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kundi linaloongoza maandamano hayo , Swaziland Solidarity Network, Lucky Lukhele, amesema mtu moja amefariki kufutia makabiliano ya jana raia wengine wakipokea matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa.

Hata hivyo vyaanzo vya taarifa kutoka kwa serikali vimekanusha taarifa kuwa mfalme Mswati wa tatu ameikimbia nchi kufutia maandmano hayo.

Licha ya serikali kupiga marufuku maandamano, wandamanaji wamekuwa wakiendelea na maandamano wengi wao wakiwa vijana.

Wandamanaji wanamtaka Mfalme Mswati wa tatu kuacha madaraka, ikiwa ni hatua ya kuelekea kwa demokrasia, na pia kuruhusu uchaguzi wa huru na haki kufanyika.

Mfalme Mswati aliyetawazwa kuwa mfalme mwaka 1986, akiwa na umri wa miaka 18, amekuwa akikashifikiwa na raia wa kawaida kwa kuishi maisha ya kifahari, huku raia wakiendelea kuzama katika lindi la umaskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.