Pata taarifa kuu
Swaziland-Uchaguzi

Wananchi Swaziland wapiga kura kuchagua wabunge, Mfalme Mswati asema utajenga demokrasia

Wapiga kura nchini Swaziland wameanza zoezi la upigaji kura hii leo Ijumaa kuchagua wabunge licha ya kukosolewa kwa uchaguzi huo kuwa unalenga kulinda maslahi ya mfalme Mswati wa Tatu.

Mfalme wa Swaziland Muswati wa III
Mfalme wa Swaziland Muswati wa III Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Katika uchaguzi huo wapiga kuwa wanatarajia kuwachagua watunga sheria wapatao 55 ambao majina yao yalipitishwa na viongozi machifu wa kimila wanaotii utawala wa kifame katika nchi hiyo masikini.

Wakati zoezi hilo likifanyika si wapiga kura wote 415,000 wanaunga mkono uchaguzi huo ambao Mswati ameulezea kama utawala wa kifalme wenye demokrasia.

Baadhi ya wananchini nchini Swazland wanadai kuwa mfumo wa utawala uliopo sasa umepitwa na wakati na unapaswa kubadilishwa ili kujenga utawala wa kidemokrasia.

Hata baadhi ya raia wanaendelea kuunga mkono utawala wa kifalme na kusema kuwa hawataki vyama vya siasa kwani vitaivuruga nchi yao ambayo inaelezewa kuwa miongoni mwa nchi masikini duniani.

Vikundi vya upinzani kama vile chama cha Pudemo vimetoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi huo kwa sababu Mswati pekee ndiyo anayechagua viongozi wa serikali ambao wanamtii hatua ambayo ni kinyume na demokrasia.

Mswati mwenye umri wa mika 45 anadaiwa kuhodhi madaraka makubwa kuliko hata serikali na ana mamlaka ya kukubali au kukataa sheria anavyoona inafaa hatua ambayo imekua ikikosolewa.

Katika hatua nyingine mfame huyo ana mamlaka ya kuvunja bunge na hawezi kushitakiwa au kufunguliwa mashitaka na siku chache kabla ya uchaguzi huo Mfalme Mswati alichagua msichana wa miaka 18 kuwa mmoja wa wake zake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.