Pata taarifa kuu
MALI-SHAMBULIZI

Wanajeshi sita wa Mali wauawa, wengine 15 wa MINUSMA wajeruhiwa

Wanajeshi sita wa Mali wameuawa katika kijiji cha Boni  na wengine 15 wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa baada ya kulipuka kwa gari lililokuwa limetegewa bomu Kaskaini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Mali wakipiga doria katika eneo la Mopti na Djenne,  28 Februari 2020.
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria katika eneo la Mopti na Djenne, 28 Februari 2020. © AFP - Michele Cattani
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo, lililotokea katika kambi ya muda ya Jeshi  katika êneo la Tarkint.

Wizara ya Ulinzi nchini Ujerumani imesema wanajeshi 12 waliojeruhiwa ni raia wa nchi yake na watatu, wamepata majeraha mabaya.

Mali imeendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, baada ya kuzuka kwa makundi yenye silaha mwaka 2012 ambayo yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha wakiwemo wanajeshi.

Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani MINUSMA, lina wanajeshi 13,000 kutoka mataifa mbalimbali  nchini humo, ikiwemo Ufaransa lakini majihadi wameendeleza mashambulizi ambayo yamesambaa katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mapema mwezi huu, alitangaza mpango wa nchi yake kujiondoa kwenye operesheni ya kijeshi katika êneo la Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.